Posts

Showing posts from May, 2016

Tamko la ACT Wazalendo Baada ya Wabunge wa Upinzani Kufungiwa

Image
Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne. Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January. Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya…… ’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’ ’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi’ ’Tungesikitishwa

Baada ya Nay wa Mitego Kuchepuka na Msichana wa Kihabeshi… Lulu Diva Aliyekuwa Mpenzi Ahamia Kwa Belle 9

Image
SIYO siri tena! Baada ya mkali wa Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuchepuka kwa msichana wa Kihabeshi mwenye asili ya Ethiopia, aliyekuwa mpenzi wake Lulu Abass ‘Lulu Diva’ naye ameamua kugeukia kwa staa wa muziki, Abedinego Damian ‘Belle 9’. Akizungumza na Over Ze Weekend Lulu ambaye ni muuza nyago kwenye video za Kibongo alidai kuwa, Nay hajatulia na badala yake anahitaji kuwa na mtu asiye na skendo za kutembea na wanawake ovyo na Belle 9 ndiye tulizo lake. “Ni ukweli Nay nilikuwa naye kwenye uhusiano nikifahamu alishawahi kuwa na msururu wa wanawake lakini siyo siri yamenishinda na sasa nahitaji kujiweka kando. Sasa hivi feelings zangu zote zipo kwa Belle na analijua hilo,” alisema Lulu

Maalim Seif Kikaangoni LEO.....Polisi Wamtaka Aripoti Makao Makuu ya Polisi Kwa Ajili ya Kuhojiwa

Image
Baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, hatimaye hatua hiyo sasa imeelekea kutekelezwa. Taarifa rasmi ya jeshi hilo visiwani Zanzibar, imemtaka Maalim Seif afike katika Ofisi za Makao Makuu ya Polisi, Ziwani mjini hapa leo saa 4.00 asubuhi. Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa CUF, Salim Bimani alithibitisha Maalim Seif kupokea barua hiyo jana wakati akiwa njiani kuelekea Dunga, Wilaya ya Kati Unguja, akiendelea na ziara yake katika majimbo ya Unguja. “Ni kweli Maalim amepokea taarifa hiyo na ametakiwa afike Ziwani (mjini hapa) kesho (leo) saa nne asubuhi,”  alisema Bimani  Bimani aliongeza kuwa hatua hiyo ya sasa imekuja baada ya jeshi hilo kuahirisha hatua ya wito wa kumhoji Maalim Seif, Ijumaa iliyopita. Barua hiyo ya kuahirisha iliyosainiwa  na Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Mei 26, yenye kumbukumbu namba PHQ/ Z/C.5/4/4/TEMP/34 kwenda kwa Maalim Se

Mwalimu Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumkuwadia Mwanafunzi Wake

Image
Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo. Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo. Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono. Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita. “Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya Aliyetumbuliwa Jipu na Waziri Afunguka

Image
  ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.  Mgaya ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo vya uhakika katika habari zao.  “Mimi nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.  Aidha, Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuun

Diwani wa Mtibwa Ashikiliwa kwa Tuhuma za Ubakaji

Image
Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14, mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni. Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 29 saa 12 jioni kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sultan, Manispaa ya Morogoro. Matei alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo, kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo, hivyo askari walifuatilia nyendo zake na kumkamata. Alisema askari baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108. Alisema uchunguzi wa kitabibu unaendelea kuthibitisha tuhuma hizo. Akizungumza kwa simu, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhan alithibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu ni kwa tuhuma gani. Ramadhan alisema kwa sasa wao kama

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MASHIRIKA YA KUJITOLEA ILI WAJIONGEZEE UJUZI NA MAARIFA

Image
Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii. Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali. Martin alisema, “Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu”   “Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashir

China Wammwagia Sifa Rais Magufuli....Wasema Kaipaisha Tanzania Kimataifa

Image
SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania inasifika duniani. Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida. Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu bure.  “Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,”  alifafanua. Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli. “Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena iwe ni elimu bora na elimu bo

Mgambo Wa Mahakama Atupwa Jela Miaka 3 Kwa Rushwa Asimkamate Mtuhumiwa Huko Geita

Image
  Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya mwanzo Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1 na 2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo ilifunguliwa mnamo tarehe 14/1/2016.  Akisoma hukumu mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki, Hakimu Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.  Ilisisitiza Sehemu ya Taarifa hiyo kuwa kwa mujibu wa ushahidi Mtuhumiwa aliomba kiasi cha Tshs. 300,000/= na kupokea kiasi cha Tshs. 100,000/- kutoka kwa Bw. Reuben Francis Ndimila ili asimkamate mtuhumiwa aliyeruka dhamana.  Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mahakama ilimtia hatiani Mtuh

14 Mbaroni kwa Tuhuma za Ujambazi

Image
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo wanawake wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwika wilayani Moshi, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Miongoni mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10, waganga wa kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa dawa watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na kuzindika silaha zilizokuwa zikitumika katika ujambazi na wanawake wapishi wa watuhumiwa hao wakiwa mafichoni. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mtafungwa alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kufuatia msako mkali wa askari uliotokana na taarifa za siri. Mtafungwa alisema mwanafunzi wa sekondari ya Mwika, Kelvin Shayo (17) miongoni mwa matukio anayotuhumiwa kushiriki ni pamoja na la kumpora bastola yenye namba YP0466 Tz Car aina ya brown, askari mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Elib

MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL

Image
Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam. Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo. Picha ya pamoja.  (P.T)

Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe,Kisa ni Mmewe Kuoa MKE Mwingine

Image
  MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine.  Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani.  Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo.  Anayetuhumiwa kuua mumewe  Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori amekiri kuhusika.  Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliam

Symbion Yaionya TANESCO.....Yasema Maneno ya Kizushi na Ukiukwaji wa Mkataba Wanaoufanya Utaligharimu Taifa

Image
               Kampuni ya kufua umeme ya Symbion imesema maneno ya uzushi na ukiukwaji wa mikataba unaofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) utaligharimu Taifa na kulitaka shirika hilo kusema ukweli kuhusu makubaliano yao. Kampuni hiyo pia imeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka jana, kigogo mmoja wa Tanesco (ametajwa jina lakini tunalilisitiri jina lake kwa sababu hakupatikana jana) alisaini mkataba na Symbion wa kuliuzia umeme shirika hilo la umma kwa miaka 15. Taarifa iliyoletwa jana kwa vyombo vya habari na mshauri wa Symbion, Julius Foster inaeleza kuwa taarifa zote zinazotolewa na Tanesco kuhusu uhusiano wao wa kimkataba ni za uongo na zimewashtua kwa kuwa shirika hilo la Serikali halijawahi kuieleza Symbion kuhusu tuhuma hizo. “Kama itatokea suala hili likaleta mgogoro wa kitaifa, tunataka Tanesco na Serikali na yeyote yule kufafanua masuala haya kwa kiapo na mbele ya mahakimu na tutaujulisha umma kila kitu,”  inasema taarifa hiyo. “Zaidi ya barua ambayo wal

SERIKALI YAJADILI RASIMU YA KISWAHILI YA MPANGO WA KUKABILIANA NA MAAFA

Image
Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mei 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30, 2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Morogoro tare