Posts

Showing posts from December, 2016

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DEC 23,HABARI KUU 2016 MWAKA WA AJALI

Image
                    

JAJI SEMISTOCLES KAIJAGE ATEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MWEKITI WA TUME YA UCHAGUZI(NEC)

Image

ZAIDI YA MAGUNIA 102 YA MCHELE WA PLASTIKI YAKAMATWA NIGERIA

Image
Mara nyingi tumekuwa tukisikia juu ya vipodozi bandia au dawa bandia lakini masuala yanayohusu chakula bandia hayakuwa yakigonga vichwa vya habari sana hadi hivi karibuni dunia ilipopata mshtuko juu ya uwepo wa mchele wa bandia. Mchele huu wa bandia ambao umekuwa ukihatarisha afya za watu wengi hufanana sana na mchele wa kawaida kiasi kwamba ukiiangalia kwa macho huwezi kuutofautisha.  Mchele huu unaosambaa kwa kasi duniani hutengenezwa kwa plastiki na utofauti wake na mchele wa asili huonekana mara baada ya kuupika. Jana, mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria ilikamata magunia 102 ya mchele wa plastiki yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sikukuu ili kujipatia fedha nyingi zaidi. Nigeria inaendelea na uchunguzi  kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu

NENO DIKTETA UCHWARA LAMTIKISA TUNDU LISSU

Image
Kesi ya uchochezi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo upande wa Mashtaka umetoa ushahidi wa pili. Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli za kichochezi na maudhi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Shahidi huyo wa pili aliyetambulishwa kama ASP Kimweri, alisema kauli ya Lissu aliyoitoa June 28 mwaka huu kuhusu ‘Dikteta uchwara’, ililenga katika kufanya uchochezi na ilikuwa ya maudhi dhidi ya Rais na ililenga kuchochea wananchi kuipinga na kuichukia Serikali. Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwampamba, shahidi huyo aliongeza kuwa kauli hiyo ya Lissu pia ililenga katika kuhatarisha usalama wa taifa kama ingesambazwa sehemu kubwa. Naye Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alimtaka shahidi huyo kuieleza mahakama ni nani ambaye mteja wake alikuwa anamtaja kama ‘dikteta uchwara’ na taifa analolizungumzia kwenye madai yake. Akiji

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AANZA ZIARA YA UTAMBULISHO KWA KUTEMBELEA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher ole Sendeka akisalimiana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt Samwel Ndalio Thomas mara baada ya kuwasili Halmashauri hapo. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi na mweka hazina wa Halmashauri.  Mhe. Ole sendeka akisalimiana na Karani wa Fedha “Cashier” wa Halmashauri Neema Kalundwa    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri zilizofanyika. Mhe. Ole sendeka akionesha nakala ya kitabu cha Ilani ya uchaguzi ambapo amewataka watumishi kuisoma na kila mmoja kuwajibika  kwenye eneo lake la utekelezaji  kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama Cha Mapinduzi.Kushoto kwake ni  Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri. Hyasinta Kissima –Njombe  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amekutana na kufanya mazungumzo na watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri

BABA WA BEN SAA NANE AFUNGUKA

Image
SAKATA la kupotea ghafla kwa aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bernard Saanane, limechukua sura mpya, baada ya familia yake kumjia juu mwajiri wake, Chadema, kwa kile inachodai chama hicho kimeshindwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kumtafuta. Akizungumza na MTANZANIA jana, baba mzazi wa Saanane, Focus Saanane, alisema anashangazwa na hatua ya Chadema kushindwa kujitokeza hadharani  kumtafuta mwanae ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha. “Tangu mwanangu Ben amepotea, hatujawahi kumuona (Freeman) Mbowe ambaye ndiye mwajiri wake kama  amechukua hatua yoyote ya kukutana na familia yangu, tukashauriana namna ya kumtafuta. Ukimya huu umenistajabisha mno. “Nilitegemea angekuwa mtu wa kwanza kuja kwangu, tuone njia gani ambayo tunaweza kutumia kumpata Ben. Naumia mno ndugu yangu,” alisema Focus. Alimtaka Mbowe ajitokeze na kuipa familia taarifa za mahali alipo Ben, kwani wao wametawaliwa na hofu kubwa kutokana na kijana wao kutoweka aki

MEYA MWITA AWATAKA MAWAKALA WA MAEGESHO KUWA NA MASHINE ZA EFD

Image
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema halmashauri yake haitasita kuvunja mikataba ya kampuni za maegesho zinazokiuka matakwa ya mikataba ya Jiji. Mwita ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kero zinzodaiwa kufanywa na mawakala hao wakiwa katika majukumu yao huku akitolea ufafanuzi suala la upandishwaji wa ushuru wa maegesho ya magari pamoja na kampuni zinazokamata magari kinyume cha sheria. “Kampuni za maegesho zikumbuke wajibu wake kisheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mawakala wake wanafanyakazi bila ya kuwasumbua wananchi kwa lengo la kujipatia fedha,” amesema. Kuhusu ukamatwaji wa vyombo vya usafiri holela na mawakala wa kampuni za maegesho, Mwita ametoa maagizo kwamba mawakala hao wasikamate magari yaliyowekwa katika sehemu isiyo rasmi hadi ipite dakika 60. Mwita ameongeza kuwa atafanya ukaguzi juu ya utekelezaji wa maagizo hayo ifikapo january Mosi mwakani nakuwataka wananchi kuwa makini kwawatu ambao w

MWANDISHI WA HABARI WA ITV ASHIKILIWA NA POLISI JIJINI ARUSHA

Image
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV mkoani Arusha, Khalfan Lihundi, anashikiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi Usa River, wilayani Arumeru kwa tuhuma za kuandika habari zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi. Lihundi alikamatwa jana jijini hapa majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti. Mmoja wa waandishi wa habari walioshuhudia tukio hilo, Basil Elias, alisema kuwa, walipokuwa ofisini, alifika ofisa wa polisi akidai ametumwa kumfuata Lihundi kwa ajili ya mahojiano. Kwa mujibu wa Elias ambaye alimnukuu ofisa huyo wa polisi, Lihundi anadaiwa kuandika habari ya uchochezi kuhusu mgogoro wa maji bila kumhoji mkuu huyo wa wilaya. “Habari hiyo inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi, ilikuwa ni malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji katika wilaya hiyo,”  alisema Elias. Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Chama  cha Waandishi wa Habari, Mkoa wa  Arusha (APC), Claud Gwandu, pamoja na kulaani  tukio hilo, alise

JAJI MKUU AZISHUKIA MAHAKAMA ZA TZ

Image
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amewakumbusha watumishi wa mahakama nchini kutoa haki kwa wakati ili wananchi waache kuzilalamikia. Amesema tofauti na mahakama, sekta nyingine zikiwemo za elimu na afya zinatoa huduma kupitia taasisi za umma pia za binafsi akisisitiza kuwa hakuna mahakama za binafisi nchini zinazotoa huduma kwa wananchi, hivyo mahakama zinapaswa kutenda kazi zake kwa weledi kutoka haki bila ya upendeleo na kwa wakati. “Hakuna mahakama za binafsi kama zilivyo sekta zingine hivyo mtu akikosa huduma bora katika shule za serikali anaitafuta huduma hiyo katika shule za binafsi vivyo hivyo katika sekta ya afya …. lakini kwa mahakama ni tofauti ndio sababu tunajitahidi kukarabati na kujenga majengo ya kisasa ya mahakama”   amesema Jaji Chande. Jaji Mkuu Chande ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na watumishi wa mahakama kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi waliokutana katika ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mjini Sumbawanga.