Posts

Showing posts from March, 2017

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAR 28,HABARI KUU UKWELI WAJULIKANA KIFO CHA FARU JOHN

Image

Waziri Mwigulu Awaasa Askari Kutowabambikizia Watu Kesi

Image
Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma. Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu

Nape Nnauye: Matumizi ya Nguvu sana Hayalipi

Image
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote. “Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!"   Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!  pic.twitter.com/e1jYGXgmQJ — Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape)  March 27, 2017 Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali.  Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, leo mchana alitoa agizo

Polepole atolea ufafanuzi mabadiliko ya CCM ili kuondoa uzushi Kuhusu Kumpata Mgombea wa Urais 2020

Image
Mabadiliko ya Katiba ya CCM 2017 yamegusa maeneo gani? Hivi karibuni kumekuwapo maneno ya upotoshwaji juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika tarehe 12 Machi 2017. Napenda kufafanua kwa uchache maeneo ambayo yamefanyiwa Mabadiliko ili kuanzia sasa ieleweke bayana kwamba msingi wa Mabadiliko haya ni Mageuzi Makubwa ambayo yanafanywa na Chama chetu ili kuongeza tija, ufanisi, uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.   Mageuzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanalenga kutizama Uongozi (Leadership), Muundo/Mfumo (Structure/System) na Utawala (administration). Chama chetu kimetimiza miaka 40 mwaka huu (2017) tangu kuanzishwa kwake na kipindi hiki tumeazimia kwa kauli moja kukiimarisha, kukijenga na kukifanya madhubuti. Kazi hii ya Mageuzi ya CCM ilianzishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokaa katika Mkutano wake wa mwenzi Desemba 2016 na baadaye kupitishwa kwa sauti moja na Mkutano Mkuu Maa

DKT. NCHIMBI AWAAGIZA WATENDAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI MKOANI SINGIDA, AAHIDI KUWASHUGHULIKIA WASIOSIMAMIA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaagiza watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Mkoa kusimamia na kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu ya miradi yote inayotekelezwa na serikali pamoja na wahisani hasa miundombinu ya maji ambayo imekosa usimamizi wa kutosha. Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji mara baada ya kusimamia makabidhiano ya mradi wa maji ulioibuliwa na halmashauri ya Iramba kabla ya kuundwa kwa halmashauri ya Mkalama ulipo mradi wa maji wa Iguguno wenye thamani ya shilingi milioni 847,099,550 na unahudumia watu elfu kumi. Amesisitiza kuwa serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza miradi ya maji ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo miradi hiyo imekuwa haileti mafanikio yaliyotarajiwa kutokana na kukoa usimamizi wa kutosha. “Naelekeza taarifa ya miradi yote ya maji iletwe ofisini kwangu, nataka nifahamu miradi ambayo imefikia

SOMA MAGAZTI YA LEO JUMATATU MARCH 27,HABARI KUU NAPE AIBUA MTIKISIKO CCM

Image