Posts

Showing posts from May, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 15

Image

Mbunge amwaga chozi bungeni akizungumzia udhalilishaji wa watoto

Image
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Faida Bakari amemwaga chozi bungeni akielezea udhalilishaji unaofanywa kwa watoto nchini. Faida akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni jana mjini Dodoma alisema watoto wanadhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vibaya na watu wazima. Aliiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo. “Watoto wanaharibiwa mheshimiwa waziri, naomba mchukue hatua kali za kisheria kwa watu hawa. Nilienda Pemba nililia watoto wanaharibiwa maumbo. Mheshimiwa nasema kwa uchungu,”  alisema huku akilia na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuendelea kuzungumza. Alisema walimu wamekuwa wakiwadhalilisha watoto huko Pemba na kumuomba waziri ashughulikie suala hilo. “Tumrudie Mungu, unakuta mibaba mizima inawapa mimba watoto na madevu yao mengi wanawatia watoto wenzao mimba,”  alisema. Faida pia alisema wazee wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii na kuwataka Watanzania kuwatunza

Mtikisiko wa Uchumi: Benki 3 hatarini kufungwa

Image
Hali ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga Bancorp. Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria. Hali hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake (TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa uchambuzi wa The Citizen Benki hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia 63. Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka. Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanza

Hussein Machozi Asimulia Alivyofumaniwa na Mke wa Mtu na Kisha Kupewa Kichapo Nchini Kenya

Image
Msanii Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake. Hussein Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel. "Kwa hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao. "Wakatuzunguka pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na kukimbia.  "Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa m

Profesa Lipumba Asema Ilikuwa ni MZIGO Mkubwa sana Kumnadi Lowassa......Akanusha Kutumiwa na CCM Kuivuruga CUF

Image
Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa Vyama vya Siasa Prof. Ibrahim Lipumba leo May 4, 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV amesema hakuwa na namba ya Edward Lowassa wakati anajiunga UKAWA. Aidha, kwenye mahojiano hayo Prof. Lipumba amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaiongoza CUF katika kudai haki za wananchi tofauti na Maalim Seif ambaye mara kadhaa ikitokea suala hilo haonekani akisema: “Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi Mkuu tuliingia kwenye maandamano Zanzibar, lakini Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele. Prof. Lipumba amesema pia kuwa Maalim Seif amekuwa akidai kila anapokosana na mtu kisiasa kuwa mtu huyo anatumiwa na CCM akitolea mfano wa Ahmad Rashid, akisema: “Ni kawaida ya Maalim Seif, akikosana na mtu kisiasa anasema anatumiwa na CCM. Rejea mgogoro na Ahmad Rashid". Akizungumzia kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward

Walioonewa Sakata la Vyeti FEKI Wapewa Nafasi ya Kukata Rufaa

Image
Serikali, imesema watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa. Kauli hiyo, ilitolewa jana  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. “Kama mtakumbuka, uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma, ulihusisha vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita, ualimu na taaluma zingine. “Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika. “Wale watumishi 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15, mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua. “Lakini, wale wanaodai kwamba wamewekwa kw