Posts

Showing posts from June, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 18

Image

Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku). Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua. Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana  saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

TANESCO yakanusha taarifa ya kuuza mitambo ya Kinyerezi

Image
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),limekanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi iliyosema kuwa vifaa vya mitambo ya Kinyerezi hatarini kwa kuuzwa. Tanesco imekanusha taarifa hizo, kuwa si za kweli ni upotoshaji kwa umma huku shirika hilo likidai linaendele na ulipaji kodi. Advertisement ==

TAKUKURU yaisaidia Serikali kuokoa Sh53 bilioni

Image
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017. Amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno, ikilinganishwa ni Sh bilioni 7 tu zilizookolewa katika mwaka 2015/2016. Alisema hayo jana wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) Tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma. Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Serikali imeanza kupata mrejesho mzuri kwamba watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo na vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua. “Baadhi ya hatua tulizochukua ni pamoja na kuimarisha taasisi yetu ya TAKUKURU; kuimarisha matumizi ya mashine za kielektroniki ili kupunguza mianya ya kupoteza mapato; kuanzisha mahakama ya mafisadi; kusimamia nidhamu katika utumishi wa um

Jela Miaka 23 Kwa Kuiba Cheti Kidato cha Nne

Image
Mahakama  ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26). Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka  23.  Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga. Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015. Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe

Meya wa Jiji la Arusha Amtaka Mkuu wa Mkoa Amuombe Radhi

Image
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani. "Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma," alisema. Pia, alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu. "Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi

Breaking News: Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2017

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema kutokana na mwongozo

IGP Sirro afanya ziara Kibiti na Rufiji.....Atangaza msako mkali

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro  jana alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini waalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari. IGP Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi kuwa waalifu wao ni lazima watapatikana. “Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,”  alisema IGP Sirro na kuongeza; “Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwa

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu mshahara kwa miezi 10 nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge la bajeti huan

Rose Muhando Atiwa Mbaroni mkoani Singida kwa Utapeli

Image
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo. Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea. Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida. Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Singida

Lowassa, Sumaye, Mabata Watema Cheche Msibani

Image
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki ya kisiasa.  Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia.  “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure." Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “ Hata njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu  ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.”  Wakat

Ally Kessy: Wabunge Wanaotusumbua Bungeni Wapimwe Madawa ya Kulevya

Image
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara. Keissy alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge. "Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale"  alisema Keissy na kuongeza; "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye

Akamatwa kwa kumshawishi mpenzi wake ajiue kisha achangishe fedha mtandaoni

Image
Msichana mwenye umri wa miaka 20, Michelle Carter atapandishwa kizimbani Massachusetts nchini Marekani wiki hii akikabiliwa na mashtaka ya kumshawishi mpenzi wake kujiua. Carter anadaiwa kumshawishi kwa njia ya simu mara kadhaa aliyekuwa mpenzi wake, Conrad Roy III aliyefikia uamuzi wa kujiua kwa hewa ya ‘carbon monoxide’ miaka miwili na nusu iliyopita, ambapo mwili wake ulikutwa kwenye gari lake eneo la maegesho ya magari. Upelelezi umeonesha kuwa msichana huyo alikuwa akimtumia jumbe za simu mpenzi wake huyo ambaye awali alimtaka Carter kumshauri baada ya kufanya jaribio ya kujiua bila mafanikio. Jumbe hizo zilimsihi marehemu kujiua tu huku zikimtia moyo kuchukua hatua hiyo. Baada ya Conrad kujiua, mrembo huyo aliingia kwenye mtandao na kuanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kwa lengo la kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiakili akichukulia mfano wa uamuzi wa mpenzi wake huyo, hadi upelelezi ulipomuumbua na kumtia nguvuni. Hata hivyo, mwanasheria wa Boston, Peter Elikann a

Kivuko Kipya kilichozinduliwa na kukabidhiwa kwa Waziri Mbarawa

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi kutoka kwa Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko hicho mara baada ya ujenzi wake kukamilika. Akizungumza na wananchi, Prof Mbarawa jana alisema lengo la Serikali kuongeza Kivuko hicho  ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni. “Uwepo wa vivuko vitatu kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi na ikitokea Kivuko kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utaratibu wa kawaida”. Alisema Prof Mbarawa. Aliongeza kuwa ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais John Magufuli  Wizara yake itaendelea kuboresha huduma za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Lindi , Kivuko cha Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani Mwanza. Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa Mgwatu alisema Kivuko