Posts

BURUNDI YAPOKEA AWAMU YA KWANZA YA WAKIMBIZI KUTOKA TANZANIA

Image
Burundi imepokea wakimbizi 301 wanaorudi kutoka Tanzania, ikiwa ni sehemu moja ya wakimbizi elfu 12 wanaotarajiwa kurudi Burundi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Wakimbizi hao wote wanaotoka kambi ya Nduta mkoani Kigoma, walivuka mpaka kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, chini ya mchakato wa kuwarudisha kwa hiari utakaomalizika tarehe 31 Desemba, mwaka huu.   Baada ya kuwapokea wakimbizi hao, msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Bw Terence Ntahiraja ameishukuru Tanzania kwa kuwapokea warundi wanaotafuta hifadhi.

HUSSEIN BASHE ANENA KUHUSU HALI YA USALAMA...ADAI HAKUNA ALIYE NA UHAKIKA NA MAISHA YAKE

Image
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka na kuomba muongozo wa Spika kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo yanaendelea kutokea ya kihalifu hayana hitimisho lake. Bashe amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika wa bunge Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge likutane na vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio yanayoendelea kutokea. " Mhe. Spika katika taifa letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa yakitokea matukio mbalimbali ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupata taarifa sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo ambayo hayana hitimisho" , amesema Bashe. Pamoja na hayo, Bashe aliendelea kwa kusema  "sisi tunawawakilisha Watanzania milioni 50 lakini matukio haya yanayotokea yanaharibu heshima ya taifa letu ningekuomba kama utaridhia na wabunge wataniunga mkono, uitake kamati yako ya ulinzi na usalama ya bunge tukufu ikutane na vyombo vya ulinzi na usalama ili

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 18

Image

Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku). Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua. Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana  saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

TANESCO yakanusha taarifa ya kuuza mitambo ya Kinyerezi

Image
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),limekanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi iliyosema kuwa vifaa vya mitambo ya Kinyerezi hatarini kwa kuuzwa. Tanesco imekanusha taarifa hizo, kuwa si za kweli ni upotoshaji kwa umma huku shirika hilo likidai linaendele na ulipaji kodi. Advertisement ==

TAKUKURU yaisaidia Serikali kuokoa Sh53 bilioni

Image
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017. Amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno, ikilinganishwa ni Sh bilioni 7 tu zilizookolewa katika mwaka 2015/2016. Alisema hayo jana wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) Tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma. Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Serikali imeanza kupata mrejesho mzuri kwamba watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo na vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua. “Baadhi ya hatua tulizochukua ni pamoja na kuimarisha taasisi yetu ya TAKUKURU; kuimarisha matumizi ya mashine za kielektroniki ili kupunguza mianya ya kupoteza mapato; kuanzisha mahakama ya mafisadi; kusimamia nidhamu katika utumishi wa um

Jela Miaka 23 Kwa Kuiba Cheti Kidato cha Nne

Image
Mahakama  ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26). Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka  23.  Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga. Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015. Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe