BURUNDI YAPOKEA AWAMU YA KWANZA YA WAKIMBIZI KUTOKA TANZANIA

Burundi imepokea wakimbizi 301 wanaorudi kutoka Tanzania, ikiwa ni sehemu moja ya wakimbizi elfu 12 wanaotarajiwa kurudi Burundi kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Wakimbizi hao wote wanaotoka kambi ya Nduta mkoani Kigoma, walivuka mpaka kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, chini ya mchakato wa kuwarudisha kwa hiari utakaomalizika tarehe 31 Desemba, mwaka huu.
 
Baada ya kuwapokea wakimbizi hao, msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Bw Terence Ntahiraja ameishukuru Tanzania kwa kuwapokea warundi wanaotafuta hifadhi.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?