ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Nyoka anatumika kwa sababu ya maisha halisi ya mnyama huyu ambaye baada ya muda katika maisha yake huwa anavua gamba na kuota tena kuwa kitu kipya; maana yake ni maisha mazuri, maumivu wakati wa kuvua gamba na uponyaji wakati anapoendelea na maisha ya baadaye.

Kwenye huduma za matibabu na baadhi ya majeshi utaona fimbo iliyozungukwa na nyoka, utaweza kuikuta kwenye hospitali karibu zote, huduma zote za afya na sehemu nyingine nyingi fimbo hii ni alama ya Kigiriki iliyotumika kwa maelfu ya miaka inaitwa Rod of Asclepius au Staff of Asclepius. Ni fimbo ya Mungu wa Kigiriki anayeitwa Asclepius anayehusishwa na mambo ya uponyaji na matibabu.

Nyoka

Aesculapia ni nyoka waliokuwa wanatumika katika mahekalu ya kutolea matibabu, nyoka hawa walikuwa huru katika vyumba vya wagonjwa waliokuwa wamelazwa ndani toka mwaka 300.

Lakini kwa tamaduni za Wahindu suala hili limeenda mbali zaidi katika kueleza mfumo wa vyakula, maisha, matibabu ya asili na mengine mengi.

Sehemu kama Thailand nyoka wa aina hii hutumika sana kwenye matibabu ya misuli, mishipa, msongo wa mawazo na aina nyingine ya maliwazo.

Kwa Afrika ni ngumu kidogo maana elimu nyingi za kale zilifutwa baada ya ujio wa utumwa na ukoloni na hata sasa hakuna wenye hamu ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu nyoka na jinsi wanavyoweza kutumika kwenye shughuli zao za kila siku hasa matibabu na uponyaji.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?