Posts

Showing posts from February, 2016

WAZIRI DKT. MAHIGA AZUNGUMZIA MKUTANO WA WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA UZINDUZI WA BARABARA YA ARUSHA-HOLILI/TAVETA-VOI

Image

MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ma  Mwanaidi Mussa  na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji cha Nandagala wilayani  Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma za Bima ya Afya, Fe

IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA

Image
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015. Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News. Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana k

Vyuo vya ualimu vyamwagiwa fedha

Image
SERIKALI imetenga Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya ualimu nchini. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema juzi kwamba fedha hizo zinapaswa zitumike kulipia posho za kujikimu, nauli na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Alitoa taarifa hiyo juzi wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika mjini hapa. “Serikali inatambua umuhimu wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vya ualimu ni kwa sababu hiyo mwezi huu wa Februari tumetoa Sh bilioni 1.65 kwa vyuo vya ualimu 35 vya umma nchini ili kuwezesha wakufunzi na walimu wanafunzi kushiriki kikamilifu mafunzo kwa vitendo ,” alisema huku akishangiliwa. Awali, akizungumza na wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mashujaa, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha elimu na akaonya wote wanaofikiria kuwaharibia elimu watoto wa kike. “Tunataka watoto wa kike wasome wa Kitanzania wasome hadi el

SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

Image
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati)  na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow. Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za ku

MAMBO 7 USIYOFAHAMU KUHUSU KOCHA WA LIVERPOOL JURGEN KLOPP

Image
                          Klopp alijiunga na Liverpool kama kocha mpya October 8, 2015, baada ya kukubali dili la miaka mitatu kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers. Watu wengi sana wamemfahamu Klopp alipokuwa kocha wa klabu ya Borussia Dortmund. Jamaa huyu pia ni maarufu style yake ya kushangilia pindi timu yake inapofunga goli. shaffihdauda.co.tz inakuletea vitu saba (7) ambavyo inawezekana ulikuwa huvifahamu kuhusu kocha huyu wa kijerumani. 7. Anapenda kusherekea na mashabiki Akiwa Dortmund, Klopp alikuwa anawachukua wacheaji wake na kwenda nao pub wakati wa sherehe za Christmas kwa ajili ya kujumuika na mashabiki kupata kinywaji. Kitendo hicho kilimfanya kuwa mtu maarufu kwenye career ya soka nchini Ujerumani. Natumaini mashabiki wote wa Liverpool wanasubirin kwa hamu sana siku ya Christmas. 6. Elimu Klopp alimaliza Stashahada ya Science ya michezo (Sports Science diploma) kwenye chuo kikuu cha Goethe, Frankfurt mwaka 1995. Aliandika thesis yake ya mw