MAMBO 7 USIYOFAHAMU KUHUSU KOCHA WA LIVERPOOL JURGEN KLOPP

Jurgen-Klopp11
                         Image result for kocha mpya wa liverpool
Klopp alijiunga na Liverpool kama kocha mpya October 8, 2015, baada ya kukubali dili la miaka mitatu kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers.

Watu wengi sana wamemfahamu Klopp alipokuwa kocha wa klabu ya Borussia Dortmund. Jamaa huyu pia ni maarufu style yake ya kushangilia pindi timu yake inapofunga goli.

shaffihdauda.co.tz inakuletea vitu saba (7) ambavyo inawezekana ulikuwa huvifahamu kuhusu kocha huyu wa kijerumani.

7. Anapenda kusherekea na mashabiki

Klopp with players

Akiwa Dortmund, Klopp alikuwa anawachukua wacheaji wake na kwenda nao pub wakati wa sherehe za Christmas kwa ajili ya kujumuika na mashabiki kupata kinywaji.

Kitendo hicho kilimfanya kuwa mtu maarufu kwenye career ya soka nchini Ujerumani. Natumaini mashabiki wote wa Liverpool wanasubirin kwa hamu sana siku ya Christmas.

6. Elimu

Klopp

Klopp alimaliza Stashahada ya Science ya michezo (Sports Science diploma) kwenye chuo kikuu cha Goethe, Frankfurt mwaka 1995.

Aliandika thesis yake ya mwisho juu ya somo linalohusu kutembea. Hii moja kwa moja inamaanisha anafanya kitu anachokifahamu na inaweza kuwa sababu ya yeye kufanikiwa akiwa Anfield.

5. Nywele za kupandikiza

Jurgen Klopp transplant
Klopp alifuata nyayo za Wayne Rooney baada ya kuamua kupandikiza nywele (hair transplant) mwaka 2013.

“Ndiyo ni kweli, nilipandikiza nywele, nafikiri matokeo ni mazuri au unaonaje?

4. Amefanya kazi kwenye matangazo ya biashara

Klopp and car

Kocha huyo mwenye miaka 48 alionekana kwenye tangazo maarufu la television akinadi gari la kampuni ya Opel. Opel wanasema kumtumia Klopp kama balozi kuliinua mauzo kwa asilimia 35.

3. Amesha cheza soka kabla ya kuwa kocha

Jürgen-klopp

Mjerumani huyo kunawakati alikuwa mchezaji wa klabu ya FSV Mainz 05 akicheza kama striker kabla ya kubadilisha nafasi na baadaye kuwa beki wa kulia.

Baadaye aliamua kuwa kocha wa klabu hiyo baada ya kustaafu kucheza soka 2001 na akawa kocha wa Mainz 05 hadi 2008 alipojiunga na Borussia Dortmund.

2. Klopp ni kocha mrefu zaidi kwenye ligi ya EPL

Jurgen Klopp-wenger

Kocha huyu wa kijerumani ni kocha pekee kwenye Premier League ambaye anaurefu wa futi 6 na inchi 4 akifuatiwa kwa karibu na Arsene Wenger wa Arsenal wakitofautiana kwa urefu wa cm 1.91.

1. Wimbo maarufu

Klopp21Kwa mujibu wa habari kutoka jarida la Bild la Ujerumani, Klopp anafahamu vizuri wimbo wa “You’ll Never Walk Alone”.

Kabla hajatua Anfield kama kocha mpya kufuatia kupigwa chini kwa Brendan Rodgers, Klopp alikuwa akiimba wimbo wa “You’ll Never Walk Alone”.

Inaripotiwa kwamba, wimbo huo pia huimbwa na mashabiki wa Borussia Dortmund, hiyo inamaanisha Klopp siyo mgeni wa wimbo huo wa Anfield.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu