Posts

Showing posts from July, 2016

Picha 9: Rais Magufuli alivyoendelea na ziara yake Igunga na Nzega Tabora.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida. Mkoani Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015. Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016. Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igu

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 31

Image

HATIMAYE MBOWE AHOJIWA NA JESHI LA POLISI

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia  na Maendelea (Chadema), Freeman Mbowe  leo july 31 amewasili makao makuu ya jeshi la polisi kuitikia wito wa kuhojiwa na jeshi hilo huku hali ya  usalama ukiwa imeimarishwa   kabla na baada ya Mbowe kuwasili .   Mbowe akiwa na msafara wa magari nane walikutana na ulinzi huo makali ambapo  magari ya Mbowe na Wakili Peter Kibatala ambaye alikuwa na Tundu Lissu ndio yaliruhusiwa kuingia.  Gari la Edward Lowassa na viongozi wengine wamezuiwa kwenye geti la kuingia kituoni hapo ambapo geti hilo limezibwa na gari la maji ya kuwasha ili kutoruhusu gari yoyote kutoka au kuingia

Kutana na Magari Yanayopaa Angani Kama Ndege..Angalia Picha na Video Hapa

Image
Najua umezoea kuona magari yanayotumika barabarani mtu wangu ila leo July 30 2016 nakusogezea magari yenye uwezo wa kupaa kama ndege ambayo tayari yanatumika katika nchi kama Massachusetts Marekani na Slovakia Hungary.  Angalia Picha na Video ya magari haya na wewe ujionee.              

Irene Uwoya Asema Angeumudu ‘Ukuu’ wa Wilaya Kama Angepewa

Image
Msanii wa filamu Irene Uwoya amefunguka kwa kusema kuwa kama angepata nafasi ya ukuu wa wilaya basi angefanya vizuri kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuongoza. Irene Uwoyo Muigizaji huyo ameimbia Bongo5 kuwa hakuwa na matarajio yakuteuliwa lakini kama angeteuliwa angeitendea haki nafasi hiyo. “Mimi sijaomba wala sijawai kusema kama nataka hiyo nafasi, lakini kama ikitokea naiweza sana, nipo vizuri sana ndio maana hata nikathutu kugombea ubunge kwa sababu nilijua naweza kuongoza,” alisema Irene Uwoya. Muigizaji huyo mahiri aligombea ubunge wa viti maalum Tabora lakini akakosa na kuhaidi kujipanga katika uchaguzi ujao.

Live: Mahojiano ya Edward Lowassa na Tido Mhando

Image
 

Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake. “Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,”  alisema. “Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,”  aliongeza. Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais

Mtuhumiwa wa Mauaji Jijini Mwanza Auawa akijaribu Kutoroka

Image
MTUHUMIWA wa ujambazi Msafiri Suleiman maarufu kama Juma Msukuma ameuawa wakati akijaribu kuwatoroka Polisi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 28 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni katika eneo la Igoma kata ya Igoma jijini Mwanza. Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa siku hiyo alikuwa amekamatwa na Polisi akituhumiwa kufanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha akishirikiana na wenzake watatu. Aliwataja watu hao aliokuwa akishirikiana nao ambao kwa sasa wamekamatwa na polisi kuwa ni Jackson Magesa ( Nyakibimbi), Samwel Mwita na Boniphace Nyamhanga. Kamanda alisema baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na uhalifu na akakubali kwenda kuwaonesha askari sehemu aliyoficha silaha maeneo ya Buhongwa mlimani. Alisema walipofika eneo husika aliwaonesha mkasi mkubwa wa kukatia vyuma na kipande cha nondo, huku akiwathibitishia kuwa silaha alikuwa ameichimbia ardhini katika eneo hilo. “Waka

Utajiri wa Dangote Washuka...Sasa Hayupo Katika List ya Matajiri Mia Duniani..

Image
Dangote Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote, sasa anashika nafasi ya 104 kati ya matajiri duniani. Dangote ameshuka kwa mara ya kwanza kati ya matajiri bora 100 chini ya jua kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg billionaires ranking. Bloomberg wamesema kwamba Dangote ameshuka sababu kubwa ikiwa ni kuporomoka kwa thamani ya pesa ya nchi ya Nigeria, Naira. Ambayo imeshuka kutoka 198 hadi 300, na inakadiriwa kupunguza karibu robo ya utajiri wa Dangote ambaye bado anawekeza vitega uchumi mbalimbali katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania. Kulingana na ripoti hiyo ya Bloomberg billionaires, Dangote, aliyekuwa na utajiri wa dola za Marekani $15.4 billioni (Naira 3.05 trilioni) mwezi Machi mwaka huu mpaka sasa anamiliki utajiri unaofikia dola za Marekani bilioni 11.1 (Naira3.3 trillion), kwa maana tajiri kwa pesa za nchini kwao lakini maskini kwa pesa za dola ya Marekani. Pamoja na kushuka kwake lakini bado kawazidi mabilionea wenye majina makubwa akiwemo mgombea uraisi wa Marekani, Do

Lowassa afunguka mengi Leo....Adai hakuna mwenye hati miliki Ya Nchi

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowasa amemtaka Rais John Magufuli kuwa na utamaduni wa kufanya mazungumzo na wanasiasa wenzake ili kufikia muafaka wa mambo mbali mbali ya kisiasa nchini. Lowasa ameyasema hayo leo wakati wa mahojiano na Tido Mhando kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni  ya Azam. Lowasa amesema kuwa siasa ni mazungumzo na siyo kutoa tu amri kama anavyofanya Rais Magufuli. Kadhalika Lowassa amesema kila mtu ana wajibu wa kuheshimu amani ya nchi na hakuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii. “Serikali haipaswi kuwa na ghadhabu, inapaswa kuwa na tabia ya kuzungumza. Sisi sote ni Watanzania kwa nini tunaogopa kuzungumza. Mazungumzo ndiyo njia bora ya kufikia maridhiano. Pia Rais Magufuli aitazame Zanzibar, tunasikia watu wanashughulikiwa kwa njia mbalimbali, wanakamatwa, hivyo hawezi kuikwepa Zanzibar kwani hilo ni suala lake.”  alisema Lowassa. Amesema CHADEMA ipo sahihi kutangaza operesheni ‘Ukuta’ hapo

Lowassa Uso Kwa Uso na Nape Nnauye Wakati wa Kuaga Mwili wa Mwandishi wa Tanzania Daima

Image
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga.  Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho. Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini. Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa. Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema,

Kundi la Navy Kenzo Laula Marekani..Leo Kukiwasha Viwanja vya Posta Kijitonyama Jukwaa Moja na Ali Kiba na Sauti Soul

Image
Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini linaloundwa na Aika na Nahreel, Navy Kenzo, limeingia mkataba wa kuwa mabalozi wa Klobaa App ya nchini Marekani. App hiyo ya simu inatarajiwa kuzinduliwa leo katika tamasha la  'Mwendokasi Festival ' litakalofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama. App hiyo ni mara ya kwanza kuingia Afrika na inazinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Navy Kenzo watapamba jukwaani moja na wasanii mbali mbali wa Bongo kama  Ali Kiba, Sauti Soul, Christian Bella, Juma Nature, Man Fongo, Nay wa Mitego, Nuh Mziwanda, Mr Blue , Isha Mashauzi, Roma, Quick Rocka, Ruck Beibe na Wengine Wengi  ...Usikose kiingilio Buku kumi tu Mlangoni

Mbowe asakwa na polisi, hiki ndicho alichoandika..!!

Image