Posts

Showing posts from April, 2017

Kijana aliyetoka Dar hadi Arusha kwa baiskeli amezindua rasmi kitabu chake

Image
Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu ,   jana amezindua rasmi kitabu cha " KUKIWA NA FOLENI" kilichoandikwa na Wiseman Luvanda. Pia Nabii Dr.GeorDavie alimpongeza kwa kitendo chake  alichoamua kufanya kwa kuwa balozi wa barabarani  kwa kutoka Jijini Dar es salaam hadi mkaoni Arusha wa usafiri wa baiskeli Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo mtunzi wa kitabu hicho alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu  na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo. Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha " KUKIWA NA FOLENI" , ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili  ili kuweza kukisambaza nchi nzima. Tazama baadhi ya picha za tukio hili hapo chini Pichani ni Mwandishi wa kitabu hicho Wiseman Luvanda, Akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo jana Ji

MKUU WA WILAYA YA GEITA.,MWAL HERMAN KAPUFI AMEONGOZA MAMIA KUUHAGA MWILI WA ALIYEKUWA MWANDISHI WA CHANNEL TEN MKOANI GEITA VALENCE ROBERT.

Image
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Valence Robart Mulamula ukiwa nje ya nyumba yao kwaajili ya heshima ya mwisho kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makazi yake ya milele. Baba wa Marehemu wa katika kati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi. Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robart. Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ua mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita. Mwili wa Marehemu Valence Robart ukitolewa Nje. Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robart. Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji  Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robart. Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili. Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili w

Rais Magufuli na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakubaliana kukuza zaidi uhusiano na Ushirikiano wa kiuchumi

Image
Waziri Mkuu wa Shirikisho la Kidemokrasia la Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn amemhakikishia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania utakaosaidia kuleta manufaa makubwa zaidi kiuchumi na kukabiliana na umasikini wa wananchi wa nchi zote mbili. Mhe. Hailemariam Dessalegn ametoa kauli hiyo jana Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wa Tanzania na Ethiopia kupitia vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili, anayoifanya kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Miongoni mwa maeneo ambayo Mhe. Hailemariam Dessalegn alisema atatilia mkazo ni ushirikiano katika usafiri wa anga ambapo aliahidi kuwatuma wataalamu kutoka Shirika la Ndege la Ethiopia kuja nchini kushirikiana na Wataalamu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuimarisha utendaji kazi na kuikuza

RAHA ZA PWANI YAFANYIKA DMV

Image
 Bi. Grace Mgaza Sebo akiongoza mchezo wa bahati nasibu iliyofanyika leo Ijuamaa kwenye tamasha la Raha za Pwani iliyofanyika katika hoteli ya Hampton Inn College Park, Maryland  na kuhudhuriwa na wadau wa miziki hiyo wakiongozwa na Dj Moe. Picha na Vijimambo na Kwanza Production.  Mtoto Aaliyah akichanganya tiketi za bahati nasibu kusudi ya kutangazwa mshindi.  Mtoto Allan akijiandaa kumtangaza mshindi wa kwanza aliyeamka na bahati usiku huo wa Raha za Pwani.  Rose Millinga (kushoto) akiibuka mshindi wa kwanza akikumbatiana na Bi. Grace Mgaza Sebo moja ya waandaji wa tamasha la Raha za Pwani iliyofanyika siku ya Ijumaa March 31, 2017 katika hotel ya Hampton Inn College Park, Maryland nchini Marekani.  Rose Millinga akiwa na zawadi yake katika picha ya pamoja na waandaji wa tamasha la Raha za Pwani  kushoto ni Bi. Grace Mgaza Sebo na kulia ni Steven Mgaza. Wapili toka kushoto ni mtoto Aaliyah. Mratibu wa Raha za Pawani Bw. Steven Mgaza akimpongeza mshindi wa kwan