UCHUKUZI SC, TAMISEMI KAMA FAINALI KESHO

mol1
Nahodha wa timu ya Uchukuzi SC, Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mei Mosi, Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni mkuu wa benchi, Kenneth Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0.
mol2Mwamuzi Robert Mkatakiu (aliyeshika kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo Ally wa Tamisemi aliyelala chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo alionyeshwa kadi hiyo pamoja na nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol3Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na Tamisemi wakisubiri mpira wa kona upigwe na Omary Said wa Uchukuzi (haonekani pichani). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol4Kipa wa Tamisemi,, Leonard Mkinga (katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake kabla Uchukuzi hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0.
mol5Tatu Kitula (mwenye mpira) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga bao katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei Mosi dhidi ya TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
mol6Matalena Mhagama (GA) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga, pembeni ni Dora Njau (GD) wa TPDC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 33-14.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU za Uchukuzi SC na Tamisemi kesho zitacheza mchezo wao wa mwisho wa netiboli, ambao ni kama fainali kutokana na timu zote kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, kila mmoja akiwa na pointi tisa.
Netiboli inachezwa kwa mtindo wa ligi, ambapo timu hizo zinakamilisha ratiba na mmoja akimfunga mwenzake atakuwa bingwa au zikitoka sare ya idadi yeyote ya magoli, basi Tamisemi atatawazwa bingwa kwa kuwa anaidadi kubwa ya magoli ya kufunga, 94 na wenzao wana 87.
Timu ya CDA Dodoma wanafuatia wakiwa watatu baada ya kushinda mchezo mmoja, huku Tanesco na chipukizi wa TPDC wakimaliza mashindano bila kushinda mchwezo wowote. Lakini TPDC inayofundishwa na kocha mzoefu Rose Mkisi inayoundwa na wachezaji wenye umri mdogo kati ya 20-30, ndio timu changa baada na inaonyesha baada ya mwaka mmoja itakuwa tishio kwani itakuwa na uzoefu tofauti na sasa ndio wameanza mwaka huu kushiriki mashindano haya ya Mei Mosi.
Katika mchezo wa soka timu ya Geita Gold Mine itakwaana na Tamisemi kesho katika mchezo wa fainali.
GGM wametinga hatua hiyo baada ya kuwafunga Tanesco kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumaliza mchezo wa nusu fainali bila kufungana.
Penati zote nne za GGM zilifungwa na Gwetu Guvette, Oswald Binamungu, Ally Twist na Mohamed, wakati za Tanesco walizopata ni Said Kondo na Stan Uhagile, na walizokosa ni Hemed Mtumwa na Betwel Kagimbo.Nao Tamisemi waliwachapa Uchukuzi SC kwa magoli 2-0.
Katika mchezo wa netiboli uliochezwa jana jioni Uchukuzi SC waliwafunga chipukizi wa TPDC kwa magoli 33-14. Uchukuzi walikuwa mbele kwa magoli 15-8.
Nayo Tamisemi waliwapeleka jamaa zao CDA na kuwachapa magoli 18-13. Washindi walikuwa mbele kwa magoli 9-8.
Katika kamba kwa wanaume Ukaguzi waliwavuta CWT kwa mivuto 2-0, nayo TPDC wakiwavuta UDOM mivuto 2-0, na Uchukuzi SC walipata ushindi wa chee baada ya Tanesco kuingia mitini; wakati kwa wanawake Tamisemi waliwavuta bila huruma Tanesco mivuto 2-0.
Mbali na netiboli na soka itakayochezwa kesho, pia kutakuwa mechi za kamba wanaume TPDC kucheza na CWT, huku UDOM kuumana na Tanesco; wakati wanaume Uchukuzi SC watakutana na TPDC.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu