Kutana na "Mamba" Anayeweza Kutabiri Matokeo ya Uchaguzi,Anaitwa "Burt"

Mamba anayeweza kubashiri matokeo Australia 

Gazeti moja nchini Australia limedai kwamba kuna mamba anayeweza kubashiri matokeo ya uchaguzi nchini Australia.

Gazeti hilo la Northern Territory News ni maarufu kwa habari zake katika ukurasa wake wa kwanza.

Huku raia wakisubiri uchaguzi wa siku ya Jumamosi ,gazeti hilo liliweka picha za wagombea wawili wakuu wa uchaguzi huo katika ndoana ya samaki na kumrushia mamba anayeitwa Burt mwenye urefu wa mita 5.1.

Burt alionekana kuifuata picha ya kiongozi wa upinzani Bill Shorten ,lakini baada ya muda akaamua kuitia mdomoni ndoana ya picha ya waziri mkuu Malcolm Turnbull,ikiwa ishara inayoonyesha kwamba ataibuka mshindi katika uchaguzi huo.

''Wanaobashiri tayari wamesema kuwa waziri huyo ataibuka mshindi'', alisema muhariri wa gazeti hilo Matt Williams.

Ubongo wa mamba huyo ni mdogo sana lakini ni miongoni mwa wanyama werevu sana.

Mamba huyo huishi katika mbuga ya wanyama pori ya Crocosaurus Cove na alishiriki katika katika filamu ya Australia Crocodile.

Ni mnyama wa hivi karibuni aliyebainika kuwa mwerevu huku yule maarufu akiwa Pweza Paul,ambaye alifanikiwa kubashiri matokeo ya mechi saba katika kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Ujerumani.

Via>>BBC

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu