Magufuli: Kuna Mtu Alikuwa Anahamisha Kati ya Tsh milioni 7-8 kila dakika. Yuko Mikono Salama..

Jana Mtukufu wa nchi mkuu sana Rais Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya kula kiapo cha uadilifu alitamka ''Tulikuwa tunafuatilia kwenye revenue, yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha''

Kauli hii imeniacha njia panda, kwamba huyu mtu
- Alipata wapi ujasiri wa kuhamisha kiashi hicho cha fedha kila baada ya dakika moja?
- Hizo fedha zilikuwa kwa wema au ubaya?
- Huyo mtu ni nani mpaka asitajwe wananchi wakamjua?
- Yuko mikono salama, Hiyo mikono salama ni ipi kwa mtu wa namna hii?
- Watazirudisha vipi pesa zote alizohamisha?
- Amekuwa akihamisha pesa kwa muda gani na mpaka anawekwa mikono salama alikuwa kashachukua kiasi gani?
- Atapelekwa mahakama ya uhujumu/mafisadi?

By Chachu Ombara/JF

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu