UNHCR waiomba Kenya kutofunga kambi ya Daadab

Image copyright
Image captionKambi za Wakimbizi
Shirika la kimataifa la kuwasaidia wakimbizi limeitaka Kenya kuongeza muda wa kuwaondoa wakimbizi wapatao mia tatu hamsini wenye asili ya Somali.
Mkuu wa UNHCR,Filippo Grandi amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa si salama kuwaondoa kwa wingi wasomali wanaoishi Kenya katika kambi ya Dadaab kurudi nyumbani.
Hivyo amewataka wahisani kutoa misaada ya ajira na miundombinu nchini Somali ili kuwawezesha wakimbizi kurudi nyumbani kwa hiari yao.
Mwezi uliopita,Kenya ilitangaza kufunga kambi ya Dadaab ifikapo mwezi novemba.Jambo lililopelekea waziri wa mambo ya nje ya wasomali kuonya juu ya ongezeko la wafuasi wa Alshaabab.

Comments

Popular posts from this blog

Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA