Picha: Harmonize afunguka juu ya tattoo yake mpya mkononi yenye sura ya Mama yake mzazi na ile ya Diamond Platnumz
Nyota wa muziki kutoka Wasafi Classic baby (WCB), Harmonize, amechora tattoo mpya yenye sura ya Mama yake mzazi kwenye mkono wake wa kushoto.

Akipiga story ndani ya eNEWZ amesema “labda ni mapenzi ya dhati na kuamua kubadilisha muonekano kwani nilivyokuwa ni tofauti siku zinasogea na na vitu vinakuwa tofauti kwakuwa sisi vijana tunakuwa na matamanio kama nilivyotamani kuchora picha ya bi mkubwa”.

Pia Harmonize ameongelea muonekano mpya kichwani kwake uliofananisha na muonekano wa mwanamuziki wa Bongo flava Jux, mwanamuziki wa Rn’B kutoka Marekani Chris Brown na The Game baada ya kusemwa sana na mashabiki mitandaoni kuwa anaendeleza tabia yake ya kuiga iga.
Hata hivyo Harmonize aliendelea kusema kuwa kusuka ni kitu alichokuwa anakitamani na kukipenda kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wakikifanya sambamba na mfano wa yeye kuamua ku vaa kuvaa style ya riboni kichwani style iliyokuwa ya zamani saana kwa baadhi ya wasanii.
Comments
Post a Comment