IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?

african_american_bride_joshuadwain_munaluchi011-612x300

Hili ni swali kwa kila mmoja ambaye ni mwalikwa ama kwa familia inayooza ama kuozesha kijana wa kike au wa kiume. Swali hili huishia kujibiwa kwa vitendo kwani mtu hutumia muda mwingi kufikiri zawadi ya kumpa bibi harusi ama bwana harusi lakini mwisho wa siku mtu huamua kubeba chochote kitu kwa ajili ya kuwatunukia maharusi.

Zawadi za maharusi hutegemea na hadhi ama hali za familia na familia, wengine hutoa zawadi ya viwanja, nyumba, fedha taslimu, magari na hata samani za gharama kubwa ili kuiwezesha familia mpya inayokwenda kuishi maisha mapya kuwa na maisha bora.

Hivi karibuni Mfalme Abdullah bin Abdulaziz al Saud alizua mjadala na kuwaacha watu vinywa wazi baada ya kumzawadia binti yake choo cha dhahabu na shela vyenye thamani ya dola za Kimarekani 30,000,000 wakati wa kufunga ndoa.

choo-cha-dhahabu

Unaweza ukastaajabu kwanini atoe zawadi ya choo cha dhahabu? Kwanini isiwe kitu kingine; yote kwa yote Mwijuma Muumini kocha wa dunia akiwa na Double M Sound aliimba “zawadi ni zawadi usichague”na ndio maana binti wa mfalme huyo aliipokea zahadi hiyo aliyotunukiwa na baba yake.


Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA