KAMA TANZANIA INGEENDESHWA KIDIKTETA NANI ANGEPONA ?

Maana halisi ya neno “Dikteta” kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya mwaka 2013 toleo la 3 ni mtu anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa; ama kwa tafsiri nyingine ni mtu mwenye tabia ya kutaka lifanywe lile analosema bila kupingwa.

MAGUFULI NA LOWASSA

Kwa maana ya tafsiri iliyotolewa hapa kama ndivyo ingefanyika Tanzania swali linalogonga kichwani mwangu ni nani angepona ? Kuna yeyote angesalia kama nchi ingeendeshwa kidikteta? Hivi karibuni yalizuka maneno kutoka kwa vyama vya upinzani vikidai kwamba Rais Magufuli ni dikteta huku wengine wakidiriki kumwita rais “dikteta uchwara”; hivi udikteta hapa upo wapi? Ni kusimamia kanuni, sheria na taratibu za nchi? Ni kutumbua majizi na mafisadi? Ni kuwatetea wanyonge ama udikteta unaozungumzwa ni upi?

TUNDU LISSU

Hii leo Ripoti ya utafiti mpya wa Taasisi ya Twaweza ujulikanao kama“Demokrasia, udikteta na maandamano: wananchi wanasemaje”,  umekata ngebe za wale wote wanaosema Rais Dk. John Pombe Magufuli ni dikteta baada ya asilimia 58 ya Watanzania kusema rais sio dikteta.

Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu kati ya Septemba 24-29 mwaka huu yanasema watu sita kati ya 10 sawa na asilimia 58 walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika katika ripoti hiyo iliyohoji watu 1,602 wa Tanzania Bara ikieleza wananchi saba kati ya 10 wanaunga mkono demokrasia kama mfumo bora wa serikali.



Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu