MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb), (Wa kwanza kulia) akipokea maandamano katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  yaliyofanyika mkoa wa Geita. Wa pili kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb) akisalimiana na mmoja wa walemavu aliyejitokeza kushiriki katika maadhimisho ya  Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa, Mkoa wa Geita.
 Mmoja wa watumishi kutoka wizara ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano akitoa elimu kwa wanafuzi wa shule ya msingi kalangalala walipotembelea banda la wizara hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa mkoani Geita. 
Kikosi cha Brass Band kutoka Serengeti Mkoani mara kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yamefanyika mkoa wa Geita. 
Waendesha pikipiki (boda boda) mkoa wa Geita wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu