MAALIM SEIF ATEMWA RASMI SMZ

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 11 ya mwaka 1984, ambayo yatatoa nafasi na kumpa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani ambaye kwa sasa hayupo katika baraza hilo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, katika marekebisho hayo vifungu viwili vinahitaji kufanyiwa marekebisho kikiwemo cha 66 kwa kufanya marekebisho na kufuta maneno ya vyama na kiongozi wa upinzani.

maalim-seif-new-one

Akifafanua katika kifungu hicho, alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa Rais wa Zanzibar kuchagua nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza ambaye kwa sasa hayupo, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio mwaka huu, na hivyo kutopata mwakilishi yeyote na hivyo kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Haroun alisema katika mazingira ya sasa katika Baraza la Wawakilishi, hakuna kiongozi katika Baraza hilo pamoja na vyama vilivyopata wingi wa kura, hatua ambayo imemfanya Rais kushindwa kuteua wajumbe wawili katika Baraza la Wawakilishi.

‘Katika Baraza la Wawakilishi la sasa Rais ameshindwa kuteua wajumbe wawili katika nafasi kumi ambapo anatakiwa ashauriane na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa,” alifafanua na kuongeza kuwa Kifungu cha 77(2) kinafuta neno la upinzani lenye uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?