HUYU NDIYE OMOTOLA JALADE WA NIGERIA

Kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza wengi mnamfahamu kutokana na kazi zake nzuri anazozifanya kwenye filamu lakini tofauti na filamu ni mwanamuziki pamoja na kuwahi kuwa mwanamitindo.

motola

Omotola Jalade Ekeide ni msanii maarufu wa filamu kutoka Nigeria, mpaka sasa ameshafanya filamu zaidi ya 300, ameshachukua tuzo mbalimbali kwenye kipengele cha mwigizaji bora wa kike na kuwahi kuingia kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani.

Mwanamama huyu alianza kuigiza 1995 kwenye filamu ya Venom of Justice ambayo iliongozwa na Regnald Ebere. Reginald ndio aliyevumbua kipaji cha Omotola kwa kumpa msanii huyo nafasi ya uhusika mkuu kwenye filamu hiyo, mwaka 2015 Omotola alitimiza miaka 20 kwenye gemu la burudani.

OMOTOLA FAMILY

Omotola ameolewa na Ruban Matthew Ekeinde mwaka 1996 na sherehe ya harusi kufanyika kwenye ndege kutoka Lagos kwenda Benin mwaka 2011 ambayo ilihudhuriwa na familia na marafiki wa karibu, wawili hao wamejaaliwa kuwa na familia ya watoto wanne.


Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu