KOCHA WA SIMBA OMOG, ATAKA MABAO ZAIDI LIGI KUU YA TANZANIA BARA

joseph-omog
Klabu ya Simba imezidi kujikita kileleni baada ya kuichapa Mwadui FC kwa ushindi wa magoli 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, jana na ukiwa mchezo wa kwanza kupata pointi toka kwa Mwadui FC kwani Simba ilikuwa bado haijawahi kuwafunga wachimba madini hao.
Pamoja na hivyo, Kocha wa Simba, Joseph Omog amesisitiza kuwa lazima kikosi chake kihakikishe kinashinda mabao zaidi ingawa suala la viwanja vya mikoani ni tatizo.
“Viwanja vya mikoani ni tatizo kwa kweli, unaona ni kiwango duni na inakuwa ni tatizo kwa wachezaji na afya yao Lakini bado tunatakiwa kushinda mabao zaidi hasa kwa kuwa nafasi tunazipata, lazima kuzitumia,” alisema Omog.
Simba ilishinda tatu, mabao mawili yakifungwa na Mohammed Ibrahim na moja likifungwa na Shiza Kichuya wote hao walisajiliwa msimu uliopita wakitokea kwa wakata miwa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 32 huku ikiwa imecheza mechi 12 bila kufungwa na kuendelea kung’ara tu kwenye Ligi ya Vodacom Tanzania bara na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.(P.T)

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu