NSSF WANUNUA KIWANJA CHA EKA MOJA KWA MILIONI 800

Wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikihoji fedha zilizotumiwa na NSSF katika mradi wa kuendeleza mji wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, imedhihirika kuwa shirika hilo linakabiliwa na changamoto nyingine ya kutumia fedha nyingi zilizozidi kiwango katika miradi ya uendelezaji milki (majengo) nchini.

Hali hiyo imedhihirika baada ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuieleza NSSF kuwa uwekezaji wake kwenye majengo ni moja ya miradi iliyotumia fedha nyingi kiasi cha kupitiliza kiwango halisi wanachoruhusiwa.

Katikati ya wiki, PAC ilibaini kuwa NSSF kwa kushirikiana na mbia mwenza, ambaye ni taasisi binafsi, imehusika katika ununuzi wa kiwanja cha eka moja kwa thamani ya Sh. milioni 800 wakati thamani halisi ikiwa Sh. milioni 25 tu.


Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu