Posts

Showing posts from November, 2016

Tazama Video mpya ya Navy Kenzo – Feel Good Ft. Wildad (Official Music Video)

Image
Kundi la muziki kutoka nchini Tanzania, Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili Aika na NahReel jana Novemba 29 wameachia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Feel Good. Itazame video hiyo hapa chini.             

DK MASHINJI – 2020 HATUKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI

Image
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana bado yanaiumiza Chadema ambayo imesema haitakubali yaliyotokea yajirudie katika uchaguzi ujao. Katika uchaguzi huo, chama hicho kilishika nafasi ya pili nyuma ya CCM lakini kililalamikia matokeo huku kikisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi. Rais John Magufuli alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935, huku mpinzani wake, Edward Lowassa wa Chadema akipata kura 6,072,848. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hicho hakitakubali kudhulumiwa kwa namna yoyote ile ushindi “Hii inaonyesha katika nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki. Wewe umefanya mara ya kwanza, tukanyamaza, ukafanya tena mara ya pili tena kwa ubabe, tukalalamika, badala ya kusema njooni tuongee, unasema nendeni kokote. Sawa, tusubiri awamu ya tatu. Tukishindwa tutakupongeza, lakini tukishinda shughuli yake itakuwa ngumu,” amesema. Kuhusu utawala wa Rais Magufuli, Dk Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji wa utawala

HABARI KUU MAGAZETINI LEO NOV 30,SHIGONGO AMTOA MAFICHONI KINANA

Image
                     

WATU SITA 6 WAUAWA KWA AJALI YA GARI RUKWA

Image
Watu  sita wakiwamo mfungwa na wanafunzi wamekufa huku wengine wanane wakijeruhiwa, baadhi yao vibaya baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka mara nne katika Kijiji cha Kipande wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa katika barabara kuu ya Mpanda – Sumbawanga. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema ajali hiyo ilitokea saa 8.10 jana mchana katika Kijiji cha Kipande. Aliwataja waliokufa kuwa ni mfungwa wa Gereza la Kitete lililopo Nkasi, Gaudensi Nyambo (27), Gasper Malimi (18) na Kenzi Mwambige (18) wote wakiwa wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Nkasi na Ofisa Mipango wa Wilaya ya Nkasi, Godfrey Mwanansao. Alisema marehemu wawili hawajatambuliwa huku miili yote ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rukwa ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga . “Mfungwa Nyambo alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kitete wilayani Nkasi ambako alikuwa na kesi nyingine mahakamani alikufa wakati a

Maagizo Aliyoyatoa Rais Magufuli Baada ya Kufanya Ziara ya Kushtukiza Katika Gereza la Ukonga

Image
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Jumanne  tarehe 29 Novemba , 2016  amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam  na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja. Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini   Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.     ''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hil

HAWA NDIO WACHEZAJI WALIONUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE

Image
Ripoti kutoka Colombia zimeeleza kuwa wachezaji wawili wamenusurika kutoka katika ajali ya ndege ya Brazil iliyokuwa safarini kutoka Bolivia kuelekea Colombia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense. Wachezaji hao wawili kutoka timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional wamekuwa miongoni mwa watu watano walionusurika katika ajali hiyo iliyochukua uhai wa watu 76. Shirika la usimamizi wa majanga la Colombia limewataja wachezaji hao kuwa ni Alan Luciano Ruschel na Jacson Ragnar Follmann huku Marcos Danilo Padilha ambaye ni golikipa amefariki muda mfupi baada ya kuokolewa. Abiria wengine Rafael Correa Gobbato na Ximena Suarez pia wamenusurika. Tayari wahanga hao wanne wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya dharura karibu na eneo la ajali.

WAZIRI AKANA KUWA MUOGA KATIKA KUMSHAURI JPM

Image
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amesema mawaziri walioteuliwa na Rais John Magufuli si waoga na wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais katika masuala mbalimbali. Mpina aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu huku akisikitika kuwa maneno yanayotolewa dhidi ya mawaziri na manaibu na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wao ni waoga na hawamshauri Rais si sahihi. Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakibeza utendaji wa Baraza la Mawaziri na kuwaita waoga wasiomshauri Rais. “Wapo wale wenzetu wa upande wa pili ambao ni wapinzani wamekuwa wakitubeza mawaziri tulioteuliwa na Rais Magufuli kuwa tumekuwa waoga na hivyo kushindwa kumshauri na kulifanya taifa kusinyaa, hii si kweli. Nyinyi ni mashahidi, mmeona jinsi tunavyochapa kazi,” alisema. Katika kudhihirisha kuwa wanatekeleza wajibu na kumshauri Rais, Mpina alisema Serikali iliamua ku

Wizara ya Elimu yakanusha taarifa ya wanafunzi wa Diploma kuzuiwa kujiunga vyuo viku

Image
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetoa ufafanuzi kwamba haijapiga marufuku watu wenye Stashahada wenye sifa kujiunga na vyuo vikuu badala yake walichokataza ni wanafunzi waliofeli kidato cha nne na cha sita kujiunga na vyuo vikuu bila kuwa na vyeti vyenye sifa. Aidha, imesema kwa waliomaliza kupitia mfumo huo na wapo kazini ni wajibu wa waajiri wao kuhakikisha wana sifa za kazi wanazofanya na kutumia fursa hiyo kufanya mitihani ili kuwa na sifa zinazohitajika. Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya alitoa ufafanuzi huo jana Dar es Salaam kutokana na taarifa za upotoshaji zilizoenea mitandaoni kwamba serikali imepiga marufuku watu wenye Stashahada kujiunga na vyuo vikuu badala yake watakaoingia ni wenye sifa za kidato cha sita. Manyanya alisema kwa waliopo vyuoni kwa sasa wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na sifa za shahada kwa kusafisha vyeti vyao na wapewe fursa ya kufanya mitihani hiyo waliyofeli na kama wamefaulu kozi hiyo, pia wataweza

AKAMATWA NA NYAMA YA MBWA AKIWA ANAJIANDAA KWENDA KUUZA KAMA KITOWEO

Image
  Huyo ni jamaa wa makandana kijiji cha Kigugu ni mtalamu wa kutengeneza supu ya mbwa na nyama choma ya mbwa kama anavyo onekana kwenye picha hapo juu,  amekamatwa akiandaa msosi huwo tayari kwenda kuuza nyama hiyo  vilabuni Makandana Tukuyu.

HABARI KUU KATIKA MAGAZETI YA LEO NOV 29,WADAU WAMPINGA PROFESA NDALICHAKO

Image