DK MASHINJI – 2020 HATUKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana bado yanaiumiza Chadema ambayo imesema haitakubali yaliyotokea yajirudie katika uchaguzi ujao.

Image result for Dk Mashinji

Katika uchaguzi huo, chama hicho kilishika nafasi ya pili nyuma ya CCM lakini kililalamikia matokeo huku kikisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi.

Rais John Magufuli alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935, huku mpinzani wake, Edward Lowassa wa Chadema akipata kura 6,072,848.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hicho hakitakubali kudhulumiwa kwa namna yoyote ile ushindi

“Hii inaonyesha katika nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki. Wewe umefanya mara ya kwanza, tukanyamaza, ukafanya tena mara ya pili tena kwa ubabe, tukalalamika, badala ya kusema njooni tuongee, unasema nendeni kokote. Sawa, tusubiri awamu ya tatu. Tukishindwa tutakupongeza, lakini tukishinda shughuli yake itakuwa ngumu,” amesema.

Kuhusu utawala wa Rais Magufuli, Dk Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji wa utawala bora na matokeo yake yeye ndiyo amekuwa kila kitu.

“Wakati anaanza mapambano dhidi ya rushwa tuliamini angeweza kuliondosha tatizo hili, lakini hali ikawa tofauti,” amesema.

Amesema kadri siku zinavyokwenda, Serikali imeshindwa mapambano dhidi ya rushwa.

Pia, amesema katika mwaka mmoja huo wa Magufuli  ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na shughuli zote za siasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.

“Tuliposema hivi, watu wengi hawakutuelewa, lakini wakati anatuzuia tusifanye siasa, watu wengi walisema wale wanasiasa wamezidi,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?