HAWA NDIO WACHEZAJI WALIONUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE

Ripoti kutoka Colombia zimeeleza kuwa wachezaji wawili wamenusurika kutoka katika ajali ya ndege ya Brazil iliyokuwa safarini kutoka Bolivia kuelekea Colombia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense.

Wachezaji hao wawili kutoka timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional wamekuwa miongoni mwa watu watano walionusurika katika ajali hiyo iliyochukua uhai wa watu 76.

danilo-2-w700h500

Shirika la usimamizi wa majanga la Colombia limewataja wachezaji hao kuwa ni Alan Luciano Ruschel na Jacson Ragnar Follmann huku Marcos Danilo Padilha ambaye ni golikipa amefariki muda mfupi baada ya kuokolewa.

footballers-accident-2000x1333

Abiria wengine Rafael Correa Gobbato na Ximena Suarez pia wamenusurika. Tayari wahanga hao wanne wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya dharura karibu na eneo la ajali.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu