WAFANYAKAZI BORA WA KAMPUNI YA ZOLA WAKABIDHIWA TUZO ZA MWAKA


Bw. Emmanuel Mesilal akipokea tuzo yake ya mtoa huduma bora wa mwaka kwa mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya ZOLA wamekabidhiwa Tuzo na zawadi  mbalimbali kutokana na utendaji wao wa kazi katika sherehe maalumu iliyofanyika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo jijini Arusha mapema jana jioni.

Tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya pili tangu kampuni hiyo kuwa na makao makuu jijini Arusha Tanzania zilishirikisha wafanyakazi wake kutoka nchi jirani ya Rwanda ambapo mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Wayne Hartmann amesema kampuni  imekua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na hapo awali.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ZOLA Bw.Wayne Hartmann akifungua rasmi shughuli ya utoaji wa Tuzo za wafanyakazi bora ukumbini hivi karibuni
Bw. Wayne Hartmann ameongeza kuwa kampuni imeweza kupata wateja wapya  kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka jana kwani kwa sasa kuna mabadiliko na kampuni imeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kuwatunuku wafanyakazi walioweza kufanya kazi kwa bidii  mpaka kufikia malengo yake.

Mmiliki wa kampuni hiyo Bw.Xavier Helsegen amepata nafasi ya kuhudhrulia katika sherehe hiyo na amesema kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa  kampuni hiyo ni kuzalisha nishati ya umeme kwa ajili ya kusaidia watu kutoka gizani na kwendaa kwenye mwanga.
Mmiliki wa kampuni ya ZOLA Akizungumza  na wafanyakazi pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika Tuzo za wafanyakazi bora wa mwaka.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa wafanyakazi wamekuwa wakijituma kuhakikisha kampuni inafikia malengo kwa wakati kwani mpaka sasa kampuni imefanikiwa kwa kiasi fulani japo inakumbambana na changamoto mbalimbali.

Naye bw. Charles Mlawa ambaye ameshinda tuzo ya muuzaji bora wa mwaka(SALES PERSON OF THE YEAR) aliyeshiriki kutoka mkoani Mbeya amesema kuwa amefanya kazi kwa kujituma na ameshinda tuzo hiyo kutokana na bidii yake japo amekumbana na changamoto nyingi ikiwemo kuwafikia wateja kwa wakati.
Mshindi wa tuzo ya muuzaji bora wa mwaka kutoka mbeya Bw.Charles Mlawa

Zola ni kampuni inayotoa huduma ya nishati ya umeme wa jua hapa nchini na imefika katika zaidi ya mikoa 15 Tanzania ikiwemo Arusha,Mwanza,Mbeya,Shinyanga pamoja na Geita.
Sherehe za utoaji wa Tuzo kwa wafanyakazi hufanyika kila mwisho wa mwaka kwa lengo la kuwatunuku zawadi mbalimbali wafanyakazi wa kampuni hiyo ili waongeze ufanisi katika utoaji wa huduma ya nishhati hapa nchini.

Jiunge na Zola sasa ubadilishe maisha yako.



Comments

Popular posts from this blog

Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA