MHUBIRI ALIYEKUWA NA WAKE 86 AFARIKI NIGERIA

Mohammed Bello Abubakar huenda alikuwa na zaidi ya wake 1
Haki miliki ya picha
Image captionMohammed Bello Abubakar huenda alikuwa na zaidi ya wake 100

Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.
Wengine wao walikuwa wajawazito.
BBC iliripoti mwaka 2008 kuwa alikuwa na takriban watoto 170 lakini gazeti hilo lilisema kuwa aliwaacha watoto 203.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu