TEACHERS JUNCTION: TUNAITENGENEZA THAMANI YA MWALIMU

Imeelezwa kuwa Changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wanaochukua mafunzo ya ualimu kisaikolojia huwa wameandaliwa kuajiriwa Serikalini kitu ambacho hakitokei kwa wote na kupelekea wengi wao kukata tamaa na kuichukia taaluma hiyo.

njama-1

Kwa kuliona hilo Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na kutengeneza thamani ya Mwalimu na Taaluma ya ualimu (TEACHERS JUNCTION) imeweza kusajili walimu 1240 katika taasisi hiyo katika Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.

Akizungumza na wanahabari Meneja Miradi wa Taasisi hiyo Salum Njama amesema kuwa ili kumuandaa Mwalimu kukabiliana na Changamoto zote za taaluma hiyo wanawafuata walimu vyuoni kwa muelekeza vitu gani vya kuzingatia ili kuwa na ubora unaotakiwa.

“Tunawafuata hawa walimu wakiwa vyuoni ili kuzungumza nao na kuwaelekeza vitu muhimu vya kuzingatia akiwa chuoni ili vimtengeneze yeye kuwa mwalimu bora popote atakapo hitajika iwe Serikalini au shule binafsi”. Alisema

waandishi-junction

Aidha Njama ameishauri Serikali kutengeneza usimamizi mzuri kwa Taasisi zinazoendesha mafunzo ya ualimu kwani nyingi zimekuwa zikifanya biashara bila kungalia ni aina gani ya Mwalimu anatengenezwa na Je, atakidhi vigezo.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA