KIKWETE – TANZANIA ITAANZA KUVUMA KIMATAIFA KUPITIA MICHEZO

Image result for kikwete

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amesema muda si mrefu Tanzania itaandikwa na wino wa dhahabu kwenye sekta ya michezo.

Kikwete aliyasema hayo katika fainali za michuano ya mpira wa kikapu kwa vijana zilizofanyika kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.

“Kituo hiki kwa sasa kina vijana 50,000 wanaojiendeleza kwa soka na mpira wa kikapu, wachezaji wawili wamechaguliwa timu ya soka ya taifa,” alisema.

Image result for kikwete

“Naamini msimu ujao wa ligi vijana wengi watasajiliwa na klabu za Ligi Kuu na hata kwenye mchezo wa Kikapu… ni matarajio yangu miaka mitano au 10 ijayo Tanzania itaandikwa kwenye kitabu cha dhahabu katika medali ya soka kwani tutatoa akina Samatta (Mbwana anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji), akina Hashim Thabiti (anayecheza kikapu Marekani) kwa maana nyingine tutaondoka kuwa wasindikizaji katika mashindano ya kimataifa na kuacha kuwa kichwa cha mwendawazimu,” alisema.

Aidha Rais Kikwete alisema katika uongozi wake amejitahidi kuhakikisha michezo inakua kwa kutengeneza mazingira bora kwa kuwalipa walimu wa kigeni wa timu za taifa.

Akizungumzia fainali hizo ambazo timu ya shule ya msingi ya Lord Baden iliifunga Tusiime vikapu 22-18, Kikwete alisema michuano hiyo ya vijana itazalisha wachezaji bora kama Alana Benard wa Marekani ambaye yupo nchini kwa sasa.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

IPI ZAWADI SAHIHI KWA MAHARUSI?

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA