Posts

Showing posts from February, 2017

ZITO ANENA MAZITO KUHUSIANA NA KESI YA GODBLESS LEMA

Image
Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe Katika mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi. "Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi"  Ameandika Zitto Kabwe Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema jana baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipe

RIDHIWANI KIKWETE ASIMULIA JINSI ALIVYOPIGIWA SIMU NA BABA YAKE BAADA YA KUPIGA PICHA NA LOWASA

Image
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza uhusiano uliopo kati ya baba yake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa bado ni maswahiba. Ridhiwani ametoa ufafanuzi huo kutokana na imani iliyojengeka kuwa kuna uhasama kati ya Dkt. Kikwete na Lowassa ambao awali walikuwa maswahiba wakubwa kabla ya siasa kuingiza doa kwenye uhusiano huo.  Uhasama huo uliaminika kuwepo na kuongezeka hasa baada ya Dkt. Kikwete kuongoza kamati ya maadili ya CCM iliyoliondoa jina la Lowassa katika orodha ya waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais, hali iliyopelekea mwanasiasa huyo kuhamia Chadema na kugombea nafasi hiyo. Akizungumza wikendi hii na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo baada ya kuenea mitandaoni picha inayomuonesha akisalimiana na kuteta na Lowassa, Ridhiwani alieleza kuwa hakuna uhasama kati ya baba yake na mwanasiasa huyo mkongwe kama wengi wanavyoamini. Aliongeza kuwa amewahi kuwashuhudia wakizungumza n

CHADEMA WAIMARISHA ULINZI KWA MAMA WEMA, NI BAADA YA NYUMBA YAKE KUPIGWA MAWE

Image
Nyumba ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu. Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa. Baada ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi. ”Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira”  amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob. Meya alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegundua wanachama hao

MAKONDA ANYANG'ANYA ARIDHI NA WAZIRI LUKUVI

Image
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema itamchukulia hatua muwekezaji aliyetoa ardhi kwa serikali ya mkoa wa dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, kwa madai kuwa ardhi aliyoitoa siyo yake. Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa muwekezaji huyo aliidanganya serikali pamoja na kumdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye ndiye aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya serikali. Mbali na kosa la kuidanganya serikali, Lukuvi pia alisema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki ardhi kinyume cha sheria. Kuhusu Mkuu wa Mkoa , Paul Makonda, Lukuvi alisema tayari amekwishafanya naye mawasiliano na kumuelewesha kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda, huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya serikali. Siku ya Jumanne wiki iliyopita Makonda alikabidhiwa ekari 1500 za ardhi na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya ujen

MBUNGE WA KOROGWE AWAOMBA WANANCHI WAMPIGE MAWE

Image
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, ametoa ruhusa kwa wakazi wa jimbo lake kumwadhibu kwa kumpiga mawe iwapo atashindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015. Majimarefu aliyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Vijiji vya Kwemshai, Ngulu na Mlungui, katika ziara yake jimboni mwake. Alisema licha ya kuwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini baada ya afya yake kuimarika amerejea nchini akiwa tayari kutatua kero za umma. Aidha, amewaomba wapigakura wake kuendelea kushirikiana naye huku wakimpatia muda kumwezesha kuwatatulia kero hizo.   “Nawashukuru kwa kuniombea pale nilipokuwa nikiugua, nilikuwa nje ya nchi kwa matibabu sala zenu zimeniwezesha kuungana nanyi leo," alisema. Aliwaeleza wananchi wa Kijiji cha Mlungi kuwa tatizo la maji na umeme viko mbioni kutatuliwa ndani ya mwaka huu na kwamba wale wanaoeneza maneno kuwa hakutafanyika kitu w

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

Image
Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine.  Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.  Mk

MKUU WA WA MAJESHI AFUKUZWA KAZI GAMBIA

Image
Image caption Mkuu wa majeshi Ousman Badjie afutwa kazi Gambia Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie. Jenerali Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute. Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana. Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.

TRUMP AONGEZA BAJETI YA JESHI KWA KIASI CHA DOLA BILIONI 54

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Trump kuongeza bajeti ya jeshi kwa dola bilioni 54 Rais wa Marekani Donald Trump amaeahidi kile alichokitaja kuwa nyongeza ya kihistoria kwa bajeti ya jeshi la Marekani. Maafisa wa ikulu ya White House wanasema kuwa bajeti ya ulinzi nchini Marekani itaongezeka kwa dola bilioni 54, ikiwa ni karibu asilimia 10. Trump aahidi kuunda silaha zaidi za nyuklia Trump aitaka Marekani kuboresha silaha za nuklia Fedha hizo zitapatikana kwa kupunguza bajeti za programu zisizo za kijeshi, ikiwemo misaada ya kigeni na fedha zinazotumiwa kwa utunzi wa mazingira. Mipango hiyo itawasilishwa kwa bunge la Congress mwezi ujao. Wakati huo huo idara ya ulinzi imewasilisha kwa White House, mipango ya kulishinda kundi la Islamic State ambayo Rais Trump alikuwa ameitaka idara hiyo kuishughulikia. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Marekana inatumia fedha nyingi zaidi kwa ulinzi kuliko nchi yoyote

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEB 28,HABARI KUU,WAFANYAKAZI WA MANJI WANASWA WAKITOROKA

Image

LORI LAPINDUKA NA KUUA WAFANYABIASHARA 6 NA KUJERUHI 12

Image
Wafanyabiashara sita wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya lori lililokuwa likiwapeleka mnadani kuacha njia na kuporomoka kwenye mlima wenye kona nyingi zinazofikia 99 wilayaniLushoto.  Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba zilisema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili jioni katika mlima wenye idadi hizo za kona zinazoanzia Mng’aro hadi Mlalo wilayani Lushoto, baada ya lori aina ya Mitsubishi Fuso Canter kuporomoka.  Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema lori hilo lilikuwa likitokea Kijiji cha Mng’aro kilichopo uwanda wa chini lilipokuwa likipanda mlima kuelekea Mlalo kwa ajili ya kuwahi soko siku inayofuata.  Walisema lori hilo lilipofika katikati ya mlima liliacha njia na kurudi nyuma hatimaye likaporomoka bondeni, huku mizigo ikiwaangukia watu hao.  Kamanda Wakulyamba aliwataja waliokufa kuwa ni Jamal Hemed (40), mkazi wa Mlalo, Hassan Rashid (33) wa Nyasa, Bisura Seif wa Kifungilo, Hadija Sai

TAASISI YA SEKTA BINAFSI YAJIPANGA KUWAJENGEA UWEZO WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI

Image
TAASISI ya sekta binafsi nchini (TPSF) imetoa wito kwa wahitimu na vijana waliopo vyuoni kuchangamkia fursa ya mpango maalum uliobuniwa baina yake na Serikali ambao umekusudia kuwajengea ujuzi kabla ya kuajiriwa ili waweze kufanya kazi kwa weledi. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu wahitimu wa vyuo vikuu kushindwa kuonyesha ujuzi baada ya kuajiriwa. “Upo upungufu mkubwa wa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wengi wanaomaliza vyuo vikuu nchini na imedhihirika kuwa wahitimu hao hushindwa kufanya kazi kwa weledi wanapokuwa wameajiriwa na sekta mbali mbali. Alisema kuwa mpango huo maalum umeanzishwa kwa lengo la kuwatayarisha wahitimu wa vyuo kupata mafunzo ya muda mfupi ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapoajiriwa au kutaka kujiajiri. Simbeye alisema Mpango huo pia umekusudia kuwapunguzia gharama waajiri, hasa wa sekta binafsi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakitumia

HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZAAGIZWA KUWASILISHA TAARIFA ZA MAENDELEO YA MPANGO WA BIASHARA NCHINI

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.   Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongo