Posts

Showing posts from June, 2016

Magufuli: Kuna Mtu Alikuwa Anahamisha Kati ya Tsh milioni 7-8 kila dakika. Yuko Mikono Salama..

Image
Jana Mtukufu wa nchi mkuu sana Rais Magufuli wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya kula kiapo cha uadilifu alitamka ''Tulikuwa tunafuatilia kwenye revenue, yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha'' Kauli hii imeniacha njia panda, kwamba huyu mtu - Alipata wapi ujasiri wa kuhamisha kiashi hicho cha fedha kila baada ya dakika moja? - Hizo fedha zilikuwa kwa wema au ubaya? - Huyo mtu ni nani mpaka asitajwe wananchi wakamjua? - Yuko mikono salama, Hiyo mikono salama ni ipi kwa mtu wa namna hii? - Watazirudisha vipi pesa zote alizohamisha? - Amekuwa akihamisha pesa kwa muda gani na mpaka anawekwa mikono salama alikuwa kashachukua kiasi gani? - Atapelekwa mahakama ya uhujumu/mafisadi? By Chachu Ombara/JF

Serikali: Hakuna Nafasi ya Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Kubadili Mchepuo au Shule

Image
SERIKALI imesema shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, zimejaa hivyo hakuna nafasi ya mwanafunzi kubadilishiwa shule au mchepuo aliochagua. Hayo yalibanishwa jana katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari mjini hapa na Msemaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rebecca Kwandu. Kwandu alisema baada ya serikali kutangaza wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, baadhi ya wazazi na wanafunzi wamekuwa wakifika ofisi za Tamisemi kuomba kubadilishiwa shule au tahasusi (michepuo) walizochaguliwa. “Tunapenda kuwaarifu kwamba shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2016 zimejaza, hivyo hakuna kinachoweza kubadilishwa,” alisema Kwandu. Aidha, Kwandu alisema vigezo ambavyo vilitumika katika uchaguzi huo ni pamoja na ufaulu na uchaguzi wa wanafunzi wenyewe juu ya masomo wanayopenda kuendelea nayo kidato cha tano na sita. “Kulingana na utaratibu uliowekwa na serikali, mwanafunzi

Milioni 800 Zatengwa Kuwasaidia Waathirika wa UKIMWI Nchini

Image
ZAIDI ya Sh milioni 800 zinatarajiwa kukusanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Virusi Vya Ukimwi mwaka huu. Fedha hizo zitakusanywa kupitia kampeni maalumu ya kupanda mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kill Challenge inayofanyika kwa mwaka wa 15, ambayo kwa mwaka huu wapanda mlima 100 wamejitokeza kushiriki. “Mgodi wa Geita kwa kushirikiana na Tacaids unatarajia kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kundi lingine la waendesha baiskeli 50 linataraji kuzunguka mlima huo kwa ajili ya kukusanya fedha hizo,”  alisema Meneja Mawasiliano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga. Tenga alisema kampeni hiyo ya Kili Challenge inaongozwa na Balozi wake, Mrisho Mpoto ambaye ni msanii wa kughani mashairi na upandaji huo wa mlima utafanyika Julai 16 na kumalizika Julai 22, mwaka huu. Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne,

Wabunge Wataka Clouds Tv Iadhibiuwe Kwa Kufanya Mahojiano na Kijana Ambaye ni SHOGA

Image
WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja. Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga. “Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,”  alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo. Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia kitendo kile, na jam

Gesi Iliyogunduliwa Tanzania Yazua Mjadala Mzito

Image
Wakati Rais John Magufuli akiungana na Watanzania wengine wanaofurahia kugunduliwa kwa gesi ya helium nchini, baadhi ya wataalamu wa miamba wameshauri uchunguzi zaidi ufanyike ili kuthibitisha uwepo wa kiasi hicho. Juzi, kulikuwa na taarifa za watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway kuwa wamegundua uwepo wa takriban futi 54 bilioni za ujazo za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya helium katika Bonde la Ufa, Kusini mwa Tanzania. Katika ukurasa wake wa Tweeter, Dk Magufuli alisema ni jambo la kumshukuru Mungu huku akiwataka wachumi, wanasheria na Watanzania kwa ujumla kujiandaa. “Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya helium, wito wangu kwa wachumi, wanasheria na Watanzania wote kwa ujumla tujipange. Ugunduzi huu utuelekeze kujipanga hasa katika eneo la mikataba yetu ili rasilimali hii adimu isaidie kuujenga uchumi wetu,” alisema. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospe

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 30

Image

Kutana na "Mamba" Anayeweza Kutabiri Matokeo ya Uchaguzi,Anaitwa "Burt"

Image
Mamba anayeweza kubashiri matokeo Australia  Gazeti moja nchini Australia limedai kwamba kuna mamba anayeweza kubashiri matokeo ya uchaguzi nchini Australia. Gazeti hilo la Northern Territory News ni maarufu kwa habari zake katika ukurasa wake wa kwanza. Huku raia wakisubiri uchaguzi wa siku ya Jumamosi ,gazeti hilo liliweka picha za wagombea wawili wakuu wa uchaguzi huo katika ndoana ya samaki na kumrushia mamba anayeitwa Burt mwenye urefu wa mita 5.1. Burt alionekana kuifuata picha ya kiongozi wa upinzani Bill Shorten ,lakini baada ya muda akaamua kuitia mdomoni ndoana ya picha ya waziri mkuu Malcolm Turnbull,ikiwa ishara inayoonyesha kwamba ataibuka mshindi katika uchaguzi huo. ''Wanaobashiri tayari wamesema kuwa waziri huyo ataibuka mshindi'', alisema muhariri wa gazeti hilo Matt Williams. Ubongo wa mamba huyo ni mdogo sana lakini ni miongoni mwa wanyama werevu sana. Mamba huyo huishi katika mbuga ya wanyama pori ya Crocosaurus Cove na alishiriki katika katika filam

CHOICE FM NA AFRICAN LYON WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA VIPAJI NA KUBORESHA MISINGI YA UENDESHAJI WA TIMU.

Image
Mtangazaji  wa Choice Fm cha Dar es Salaam, Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla yakuingia makubaliano kati ya Timu ya mpira wa miguu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara (Vodacom Premier League) na kituo cha radio cha Choice FM 102.5, juu ya ushirikiano katika kukuza vipaji na kuboresha misingi ya uendeshaji wa timu, wengine kushoto kwake alievaa kanzu ni  Mmiliki wa klabu ya  African Lyon ,  Rahim Kangezi, na Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Choice FM . Mkuu wa Vipindi Choice FM, Antonio Nugaz (kulia) akitolea ufafanuzi makubaliano hayo ambapo amesema yanalenga kujenga  mazingira ya kuweza kutambua na kuvikuza vipaji vya wanamichezo hasa wale wa mpira wa  miguu (kushoto), Mmiliki wa klabu ya African Lyon ,  Rahim Kangezi Amesema  makubaliano hayo yataiwezesha Africani Lyon yenye masikani yake Mbagala kushirikiana na  Choice FM  katika kuandaa mashindano na programm zin

MAKAMU WA RAIS AFUTURU NA WATOTO YATIMA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show. Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine. Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia)  mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni M

Dkt. Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda..!!

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili, pamoja na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili.  Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani.  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo, akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo. Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia)