Posts

Showing posts from September, 2016

Serikali Yaridhia Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Bomba La Mafuta

Image
SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.  Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika  tarehe 29 Septemba, 2016  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.  Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.  Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania.  Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.  Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye uref

SUDAN YATUHUMIWA KUTUMIA SILAHA ZA SUMU

Image
Serikali ya Sudan imefanya mashambulizi 30 yanayoshukiwa kuwa ya silaha za sumu katika eneo la Jebel Marra jimboni Darfur tangu Januari mwaka huu ikitumia kile watalaamu wamesema ni kemikali ya kusababisha malengelenge Amnesty International imekadiria kuwa karibu watu 250 huenda walifariki kutokana na silaha za kemikali. Shambulizi la karibuni kabisa lilifanyika Septemba 9 na Amnesty imesema uchunguzi wake ulizingatia picha za satelaiti, mahojiano na zaidi ya watu 200 na watalaamu kuchunguza picha zilizoonyesha majeraha. Mkurugenzi wa utafiti wa migogoro wa shirika la Amnesty International Tirana Hassan amesema matumizi ya silaha za sumu ni uhalifu wa kivita ""wakati wa mashambulizi haya, mamia ya raia walipigwa risasi, maelfu walipoteza makaazi, na moja ya mambo yanayokasirisha zaidi katika mgogoro wa Darfur ni kuwa tumepata ushahidi wa kuaminika kuwa serikali ya Sudan imekuwa ikitumia silaha za sumu dhidi ya raia" Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa Omer D

MAALIM SEIF ATEMWA RASMI SMZ

Image
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 11 ya mwaka 1984, ambayo yatatoa nafasi na kumpa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani ambaye kwa sasa hayupo katika baraza hilo. Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, katika marekebisho hayo vifungu viwili vinahitaji kufanyiwa marekebisho kikiwemo cha 66 kwa kufanya marekebisho na kufuta maneno ya vyama na kiongozi wa upinzani. Akifafanua katika kifungu hicho, alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa Rais wa Zanzibar kuchagua nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza ambaye kwa sasa hayupo, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio mwaka huu, na hivyo kutopata mwakilishi yeyote na hivyo kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Katibu Mkuu wa C

MAJALIWA KUHAMIA DODOMA LEO

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuhamia rasmi leo mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Julai 25, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imeandaa mapokezi ya Waziri Mkuu atakapowasili mchana na kuanzia kesho atafanya ziara ya siku mbili katika manispaa ya Dodoma kukagua hatua za maandalizi ya kupokea ujio wa Serikali. Taarifa ya ofisi ya mkoa imesema Majaliwa atatembelea maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji cha Mzakwe na maeneo ya viwanda. Ofisa habari wa mkoa, Jeremiah Mwakyoma amesema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi hayo yamekamilika.

TAASISI YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU – NIMR YAANDAA KONGAMANO LA WATAFITI

Image
Dk. Mwele Malecela Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kongamano kubwa la watafiti litakalofanyika tarehe 4 mpaka 6 Oktoba 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Dk. Mwele Malecela Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akizungumza nao leo, Kulia ni Dk. Julius Massaga Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti/Mtafiti Mkuu wa NIMR. Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ilianzishwa kwa Sheria namba 23 ya mwaka 1979.  Katika kipindi cha miaka 29 iliyopita Taasisi imekuwa ikiandaa Kongamano la sayansi kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha watafiti, watoa huduma za afya,  watunga sera, wakufunzi, wahisani na wadau wengine wa afya kuwasilisha na kujadili matokeo ya tafiti mbalim

PROF TIBAIJUKA AKATAA TUZO YA MILIONI 200

Image
Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ametunukiwa tuzo ya heshima ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalfa bin Salman Al Khalifa ikiwa ni utambuzi wa mchango wake wa kuchochea maendeleo. Tibaijuka ameyasema wakati akizungumza na wanahabari kwa lengo la kuelezea namna alivyopatiwa tuzo hiyo pamoja na fedha kiasi cha dola laki moja ambayo amekataa kuichukua kutokana na hofu ya kukumbwa na kashfa kama ile iliyomkumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne. Aidha amesema kuwa tuzo hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Bahrain na hutolewa baada ya miaka miwili kwa mtu ambaye ametoa mchango mkubwa katika kutatua changamoto za sekta mbalimbali za kiuchumi ambazo zinawakumba wananchi. Aidha Profesa Tibaijuka amefafanua kuwa tuzo hiyo imetokana na kushughulikia malengo ya milenia wakati akiwa anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa (UN) na kusema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa watanzania kwani alie

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30

Image

SEMINA YA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA MUHIMBILI YAFANYIKA.

Image
 Mtoa Mada, Martha Mkony akizungumzia vifo vya watoto na jinsi ya kutoa huduma bora kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda na njia ya kuzuia vifo kwa watoto hao.  Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada hiyo Leo katika hospitali hiyo.  Dk Arvinder Singh akizungumzia umuhimu wa kununua vifaa tiba, kuwapo kwa madaktari na wauguzi wa kutosha, kuwapo kwa gesi ya uhakika, chumba cha kisasa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na madaktari na wauguzi kutoa huduma kwa wakati kwa watoto hao.  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.  Dk Hassan Mtani akitoa mada kuhusu kifafa cha mimba katika mkutano uliofanyika Leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

KAMA TANZANIA INGEENDESHWA KIDIKTETA NANI ANGEPONA ?

Image
Maana halisi ya neno  “Dikteta”  kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya mwaka 2013 toleo la 3  ni mtu anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa; ama kwa tafsiri nyingine ni mtu mwenye tabia ya kutaka lifanywe lile analosema bila kupingwa . Kwa maana ya tafsiri iliyotolewa hapa kama ndivyo ingefanyika Tanzania swali linalogonga kichwani mwangu ni nani angepona ? Kuna yeyote angesalia kama nchi ingeendeshwa kidikteta? Hivi karibuni yalizuka maneno kutoka kwa vyama vya upinzani vikidai kwamba Rais Magufuli ni dikteta huku wengine wakidiriki kumwita rais “dikteta uchwara”; hivi udikteta hapa upo wapi? Ni kusimamia kanuni, sheria na taratibu za nchi? Ni kutumbua majizi na mafisadi? Ni kuwatetea wanyonge ama udikteta unaozungumzwa ni upi? Hii leo Ripoti ya utafiti mpya wa Taasisi ya Twaweza ujulikanao kama “Demokrasia, udikteta na maandamano: wananchi wanasemaje”,   umekata ngebe za wale wote wanaosema Rais Dk. John Pombe Magufuli ni dikteta baada ya as

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA.

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb), (Wa kwanza kulia) akipokea maandamano katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  yaliyofanyika mkoa wa Geita. Wa pili kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani.  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (Mb) akisalimiana na mmoja wa walemavu aliyejitokeza kushiriki katika maadhimisho ya  Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa, Mkoa wa Geita.  Mmoja wa watumishi kutoka wizara ya ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano akitoa elimu kwa wanafuzi wa shule ya msingi kalangalala walipotembelea banda la wizara hiyo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa mkoani Geita.   Kikosi cha Brass Band kutoka Serengeti Mkoani mara kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yamefanyika mkoa wa Geita.  Waendesha pikipiki (boda boda) mkoa wa Geita wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalam

Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo

Image
Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema umefika wakati wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia upya sera ya ukopeshaji ili waweze kutoka mikopo kwa ngazi ya Astashada kwa masomo ya Sayansi ili kupata wataalam wengi wa fani hiyo Mhe. Mpina amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kwenda sambamba ma mapinduzi ya maendeleo ya uchumi wa viwanda jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na wataalam wengi wa mambo ya Sayansi na kuongeza tija katika ustawi wa maendeleo ya viwanda. Akiongea na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo ya elimu ya Visiwani Zanzibar, amesema Tanzania sasa inataka kuingia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji wataalam wengi wa masomo ya Sayansi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Abdul-Razaq Bandru, amesema kuwa bodi hiyo inafanya marekebisho mbalimbali ikiwemo kufanikisha mabadiliko ya kanzidata ili kuwafikia wadaiwa kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Katika hatua nyingine Naibu Waziri Luhaga ame

SERIKALI IMETOA BIL.2 KUJENGWA GATI NYAMISATI

Image
SERIKALI imeanza kutenga fedha sh. bil.2 ambazo tayari zimeshapelekwa wizara ya ujenzi ,ili kujengwa gati itakayohudumia wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti,Mafia na Rufiji. Aidha serikali inafanya utaratibu wa kutafuta boti moja kubwa ambayo itaweza kuhimili nguvu ya maji na kukatisha katika maeno hayo. Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyazungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi huko Nyamisati wilaya ya Kibiti,mkoani Pwani. Alisema serikali imedhamiria kuimarisha na kuondoa kero iliyopo kwasasa wanayopata wananchi baada ya gati la awali kubomoka kutokana na kushindwa kuhimili nguvu ya maji. Alisema kipindi cha nyuma halmashauri yenyewe ilijenga gati hiyo kwa kiasi cha sh.mil.400 lakini ilibomoka kutokana na wingi wa maji . “Wilaya ya mafia waliizungumzia vizuri sana kuwa ni tumaini lao,na mimi nilidhani watazungumzia kitu kipya lakini wameipenda sana Nyamisati,kwahiyo wakizungumza kitu ambacho nakifahamu,lakini serikali inajua gati hii inatumika na wilaya yot

Waziri Mkuu MAJALIWA APOKEA MISAADA ZAIDI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Image
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septem