Posts

Showing posts from October, 2016

HESLB Yafafanua vigezo Utoaji mikopo.........Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017. Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu. Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza. Katika mkutano na waandishi wa habari jana (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupokea maombi mwezi J

WAKAMATWA NA MAGAMBA YA KAKAKUONA

Image
WATU wanne wakiwemo raia watatu wa Burundi, wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro baada ya kukutwa na magamba ya kakakuona, yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.4. Walikuwa wamehifadhi magamba hayo kwenye mifuko 67, yakisubiri kusafirishwa kwenda nje ya nchi kuuzwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema watu hao walikamatwa saa tano na nusu usiku wa Oktoba 28, mwaka huu eneo la mtaa wa Reli, kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro. Walinaswa ndani ya ghala moja, lenye mashine ya kukoboa na kusaga nafaka. Alisema, askari wa jeshi hilo wakiwa katika msako, walipokea taarifa za kiintelejensia kutoka kwa raia wema kuhusu mazingira ya watu katika eneo hilo. Walipofika, walikuta watuhumiwa hao wanne. Baada ya upekuzi kwenye ghala hilo, polisi walikamata magamba ya kakakuona katika mifuko 67, baaadhi yake yakiwa tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Kamanda Matei aliwataja raia wa Burundi waliokamatwa kuwa ni Kibonese Golagoza ( 35)

KOCHA WA SIMBA OMOG, ATAKA MABAO ZAIDI LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Image
Klabu ya Simba imezidi kujikita kileleni baada ya kuichapa Mwadui FC kwa ushindi wa magoli 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, jana na ukiwa mchezo wa kwanza kupata pointi toka kwa Mwadui FC kwani Simba ilikuwa bado haijawahi kuwafunga wachimba madini hao. Pamoja na hivyo, Kocha wa Simba, Joseph Omog amesisitiza kuwa lazima kikosi chake kihakikishe kinashinda mabao zaidi ingawa suala la viwanja vya mikoani ni tatizo. “Viwanja vya mikoani ni tatizo kwa kweli, unaona ni kiwango duni na inakuwa ni tatizo kwa wachezaji na afya yao Lakini bado tunatakiwa kushinda mabao zaidi hasa kwa kuwa nafasi tunazipata, lazima kuzitumia,” alisema Omog. Simba ilishinda tatu, mabao mawili yakifungwa na Mohammed Ibrahim na moja likifungwa na Shiza Kichuya wote hao walisajiliwa msimu uliopita wakitokea kwa wakata miwa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro. Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 32 huku ikiwa imecheza mechi 12 bila kufungwa na kuende

PSPF YAIPONGEZA KILIMANJARO FC SWEDEN KWA KUPANDA DARAJA

Image
Timu inayoundwa na Wana-Diaspora wa Kitanzania waishio Sweden, Kilimanjaro FC, hivi karibuni imefanikiwa kupanda daraja kutoka Daraja la Saba kwenye Ligi ya Sweden ijulikanao kama Allsvenska na kufikia Daraja la Sita. Bwana Abdul Njaidi ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bwana Adam Maingu, umeipongeza timu hiyo ya Kilimanjaro FC kwa hatua hiyo kubwa na ya kutia matumaini katika kuinua soka la nchi yetu kwa ujumla. "Vijana wa Kilimanjaro FC wamekuwa mabalozi wazuri kwenye kuitangaza nchi yetu kimataifa. Sisi wa PSPF tunawakaribisha vijana wa Kilimanjaro FC na Watanzania wengine walio nje ya nchi kujiunga na mifuko yetu ya hifadhi kwa kuwasaidia wao wenyewe na ndugu na jamaa zao walio nyumbani." 

NSSF WANUNUA KIWANJA CHA EKA MOJA KWA MILIONI 800

Image
Wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikihoji fedha zilizotumiwa na NSSF katika mradi wa kuendeleza mji wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, imedhihirika kuwa shirika hilo linakabiliwa na changamoto nyingine ya kutumia fedha nyingi zilizozidi kiwango katika miradi ya uendelezaji milki (majengo) nchini. Hali hiyo imedhihirika baada ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuieleza NSSF kuwa uwekezaji wake kwenye majengo ni moja ya miradi iliyotumia fedha nyingi kiasi cha kupitiliza kiwango halisi wanachoruhusiwa. Katikati ya wiki, PAC ilibaini kuwa NSSF kwa kushirikiana na mbia mwenza, ambaye ni taasisi binafsi, imehusika katika ununuzi wa kiwanja cha eka moja kwa thamani ya Sh. milioni 800 wakati thamani halisi ikiwa Sh. milioni 25 tu.

DTB YAZINDUA TAWI LA 26 BARABARA YA MWAI KIBAKI, MBEZI CHINI, JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta, akikata utepe katika uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Diamond Trust lililopo barabara ya Mwai Kibaki, Mbezi Chini Jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Viju Cherian na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha Joseph Mabusi na Meneja wa Tawi hilo Msingo Kimune wakishuhudia. Tawi hilo ni tawi la 12 jijini Dar es Salaam na ni tawi la 26 nchini Tanzania.(picha na Mpiga picha wetu) Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta akiongea na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya Diamond Trust lililopo barabara ya Mwai Kibaki, Mbezi Chini jijini Dar es salaam, Tawi hilo ni tawi la 12 jijini Dar es Salaam na ni tawi la 26 nchini Tanzania. (picha na Mpiga picha wetu) Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Diamond Trust pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta (Hayupo pichani) aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafl

HUYU NDIYE OMOTOLA JALADE WA NIGERIA

Image
Kizuri kinajiuza kibaya kinajitembeza wengi mnamfahamu kutokana na kazi zake nzuri anazozifanya kwenye filamu lakini tofauti na filamu ni mwanamuziki pamoja na kuwahi kuwa mwanamitindo. Omotola Jalade Ekeide ni msanii maarufu wa filamu kutoka Nigeria, mpaka sasa ameshafanya filamu zaidi ya 300, ameshachukua tuzo mbalimbali kwenye kipengele cha mwigizaji bora wa kike na kuwahi kuingia kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Mwanamama huyu alianza kuigiza 1995 kwenye filamu ya Venom of Justice ambayo iliongozwa na Regnald Ebere. Reginald ndio aliyevumbua kipaji cha Omotola kwa kumpa msanii huyo nafasi ya uhusika mkuu kwenye filamu hiyo, mwaka 2015 Omotola alitimiza miaka 20 kwenye gemu la burudani. Omotola ameolewa na Ruban Matthew Ekeinde mwaka 1996 na sherehe ya harusi kufanyika kwenye ndege kutoka Lagos kwenda Benin mwaka 2011 ambayo ilihudhuriwa na familia na marafiki wa karibu, wawili hao wamejaaliwa kuwa na familia ya watoto wanne.

Sumaye adai Amepata taarifa ya Kutimuliwa Nyumbani kwake pia

Image
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kuwa baada ya kutangazwa mchakato wa kunyang’anywa shamba lake la Mwabwepande, amepata taarifa ya kutaka kuondolewa anapoishi pia. Sumaye ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa kumnyang’anya mwanasiasa huyo shamba la Mwabwepande kwa madai ya kutoliendeleza kwa muda mrefu. “Hapa ninapoishi naambiwa kuna maelekezo yametoka juu kuwa sijapaendeleza. Sasa kama sijapaendeleza mbona ninaishi hapahapa,” Sumaye amekaririwa na gazeti la Nipashe. Aidha Sumaye amesema kuwa ingawa alimsikia Waziri Lukuvi akieleza kuwa tayari wameshampa notisi ya siku 90 kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Mwambwepande, hadi jana hajaipata notisi hiyo licha ya kufanya jitihada za kuifuatilia. Alisema kuwa anashangazwa na uamuzi huo wa Waziri kwani kesi inayolihusu shamba hilo bado inaendelea mahakamani kutok

HESLB yafafanua vigezo utoaji mikopo, Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Oktoba 30, 2016). Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa. Na Mwandishi Wetu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017. Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu. Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93

Polisi Wazuia Mkutano wa Maalim Seif........Wamlinda Profesa Lipumba

Image
Wakati polisi ikizuia mkutano mkuu maalumu wa CUF uliopangwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini Tanga jana, mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alifanya usafi soko la Buguruni, huku akilindwa na jeshi hilo.  Lipumba alifanya kazi hiyo akitekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi. Msemaji wa CUF, Abdul Kambaya alisema haoni kama ni jambo la ajabu kwa Lipumba kufanya usafi wakati akilindwa. “Sioni mantiki ya swali hilo, suala la kulindwa Lipumba siyo wa kwanza,” alisema  Mapema jana, polisi mjini Tanga ilizuia mkutano uliopangwa kuhudhuriwa na Maalim Seif ambao ulipaswa kuwajadili madiwani 12 waliopigana wiki iliyopita katika ofisi za chama hicho wilayani humo, baada ya kugawanyika kuhusu uamuzi wa wenzao waliohudhuria baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12. Taarifa ya jeshi hilo ilidai kuzuiwa kwa mkutano huo ni kutokana na tisho la uvunj

Matokeo darasa la saba: Majina ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri na shule 10 bora na Ambazo Hazikufanya Vizuri

Image
Ufaulu kwa watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa. Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu,  Justina Gerald  wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam. Kati ya wanafunzi hao 10, watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani Shinyanga, wawili Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera.  Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250. “Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulik

UTANDO WA BUIBUI SAWA NA ALMASI ILIYO MCHANGANI

Image
Wahenga walisema penye miti hapana wajenzi na asiyejua maana haambiwi maana! Leo navunja sheria kwa kukwambia juu ya thamani ya utando wa buibui ambao wengi wetu huuona na kuupuuzia pasipo kujua kazi yake kwa kudhani ni uchafu usio na faida yoyote. Utafiti mpya ulioripotiwa na Gazeti la Nano Letters la Marekani unaonesha kuwa utando wa buibui ni malighafi nzuri ya kimaumbile ya kutengeneza darubini, na inaweza kutumiwa kuinua uwezo wa darubini za jadi za kuangalia vitu vidogovidogo viilivyotengenezwa kwa vioo.                          Kama bado ulikuwa hujaipata hiyo sasa ufahamu na kutilia maanani utafiti ulioongozwa na Dk. Wang Zengbo kutoka Chuo Kikuu cha Bangor cha Uingereza kwa kushirikiana na Prof. Fritz Vollrath kutoka Chuo Kikuu cha Oxford. Kutengeneza darubini kwa utando wa buibui ni rahisi sana. Watafiti waliweka utando wa buibui juu ya kitu kitakachoangaliwa, kutia kileo katika kitu hicho na utando wa buibui, halafu kuangalia kitu hiki kupitia darubini ya kawaida

Sumaye: Sirudi CCM hata waninyang’anye Mashamba Yangu Yote

Image
Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo halimtikisi. Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe iliyopangiwa kesi hiyo. “Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye anakaririwana MwanahalisiOnline. Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana. “Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye. Serikali imetangaza kuanza mchakato wa

Benk ya Twiga Bancorp Yafilisika....BoT Yachukua Usimamizi wake Kunusuru Amana za Wateja wa Benki Hiyo

Image
Benki Kuu ya Tanzania imetangaza rasmi kuchukua usimamizi wa Benki ya Twiga Bancorp kuanzia jana kutokana na upungufu wa mtaji wa benki hiyo kiasi cha kuwa na deni la Shilingi Bilioni 21. Benki Kuu pia imesimamisha shughuli zote za utoaji huduma za kibenki za benki hiyo kwa kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja kuanzia jana tarehe 28/10/2016 ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo. Maamuzi hayo yametangazwa jana jijini Dar es Salaam na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndullu mbele ya waandishi wa habari, na kusema kuwa hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 56 (1)(g)(i) na 56(2) a-d cha taasisi za fedha ya mwaka 2006. "Uamuzi huu umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki ya Twiga kut

Taarifa ya Mamlaka ya Dawa na Chakula TFDA kuhusu Dawa bandia zilizokamatwa

Image
MADAWA bandia na yasiyo sahihi kwa matumizi ya binadamu yamekamatwa maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya kufanyika ukaguzi maalum wa kutafuta dawa bandia katika maeneo hayo iliyofanyika hivi karibuni. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa kutoa Matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa uliofanyika katika mikoa ya Kanda za Ziwa na Nyanda za Juu Kusini. “Kutokana na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda za Ziwa pamoja na Nyanda za Juu Kusini wa kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya binadamu tumefanikiwa kukamata dawa bandia za aina tano ambazo zipo kwenye makundi mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)”  alisema Bw. Sillo. Aidha Bw. Sillo amesema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata dawa ya malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa katika kiwanda cha Elys Chemical  nchini Kenya na nyingine zinatengenezwa hapa nchini katika kiwanda

Waziri Mkuu: Tumieni Misikiti Kuhubiri Misingi Ya Uislamu

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake. Ametoa wito huo jana mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma.  Alisema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati. “Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,”  alisema. Waziri Mkuu alisema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema. “Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya

LINDA PENZI LAKO KWA NAMNA HII…!!

Image
Kuna sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako, uishi na mke au mume si kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria. Hivi ni vipengele baadhi tu, wanandoa na wapenzi wanapaswa kuvitambua. Kwanza kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi si lazima ufanye tendo la ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili. * UPENDO KUTOKA KWA YULE UMPENDAE. hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi, hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati yeye hana habari na wewe. * AMANI. Watu wengi wana wanaume na wanawake warembo, lakini hawafurahii mapenzi kwasababu hawana amani ndani ya nyumba. Utafurahia ut