Posts

Showing posts from March, 2016

WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI

Image
Miongoni mwa vurugu zilizotokea mji mkuu wa Bujumbura Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi. Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni "mauaji". Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha. BBC

Mwakyembe Apokea Marekebisho ya Sheria Manunuzi

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria. Akipokea taarifa hiyo jana Jijini Dar es salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe alisema taarifa hiyo ya utafiti itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi. “Mimi na wataalamu wangu tumeipokea taarifa hii, tutaiangalia na kuhakikisha tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuendelea na utaratibu unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika kwa haraka” alisema Dkt Mwakyembe. Akifafanua juu ya sheria ya manunuzi ya Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi  amesema kuwa Tume imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali. “ Tumepata maoni mengi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi ya Serikali kwa namna wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi t

Wabunge Wataka Wanaoharibu Miundombinu ya DART wachukuliwe hatua Kali

Image
KAMATI ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeiagiza serikali kuwachukulia hatua kali wale wote waliovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) na kuigeuza kuwa masoko ya bidhaa zao. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza amesema hali hiyo haivumiliki na inapaswa kukomeshwa mara moja. Kamati hiyo ilikutana kwa mara ya pili na uongozi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jana jijini Dar es Salaam. “Tumejionea katika ziara yetu tuliyoifanya katika miundombinu ya mradi kuwa baadhi ya wafanyabiashara wadogo wameivamia miundombinu na kuigeuza kuwa masoko,”  alisema. Rweikiza ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini alisema jambo hilo haliwezi kufumbiwa macho kwani mradi huo umegharimu fedha nyingi na zitalipwa na kodi ya Watanzania. Alisema pia baadhi ya madereva wa magari na pikipiki maarufu kama bodaboda wameharibu baadhi ya miundombinu na kwamba wanatakiwa kudhibitiwa. Aliitaka serikali kuweka ulinzi na wote wanaobainik

Profesa Muhongo Asema Kitendo Cha Marekani Kusitisha Misaada ya MCC Hakutaathiri Miradi ya REA ya usambazaji wa Umeme vijijini

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo amesema kuwa kwa   Tanzania  kutopatiwa  fedha na Marekani  kupitia Mfuko wa  Maendeleo  ya Changamoto za Milenia (MCC) ambazo ni Dola za Marekani  milioni 472 kwa ajili ya miradi ya  barabara,  maji na umeme hazitaathiri  miradi ya usambazaji umeme  vijijini inayofadhiliwa na  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA). Aliyasema hayo  jijini Dar es salaam wakati  akifanya majumuisho  ya vikao vyake na wakandarasi wanaosambaza umeme  vijijini  ambavyo vilianza tarehe  29 Machi, 2016 na kuhudhuriwa na watendaji wa Wizara, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na REA. Profesa Muhongo alisema kuwa fedha hizo zilikuwa haziendi moja kwa moja katika mfuko wa REA wala serikali kuu kama inavyodaiwa na watu wengi. “Zile fedha za MCC tulikuwa tunakaa na MCC, tunasema bwana katusaidie kusambaza umeme mfano Shinyanga, kwa hiyo anachukua zile fedha zake anaenda na wakandarasi wake moja kwa moja Shinyanga, huku miradi ya REA ikiendela kama ilivyopang

Jeshi la Polisi Tarime/Rorya Laanza Msako wa Wanaume Wanne Waliombaka Binti Mmoja kwa Zamu na Kumharibu Vibaya

Image
JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili katika eneo hilo. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta alisema, watu hao wanatuhumiwa kuwabaka wasichana hao katika matukio mawili tofauti yaliyotendwa kwa nyakati tofauti Machi 26, mwaka huu katika wilaya za Rorya na Tarime. Satta alisema kuwa, katika tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime (Jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka shuleni siku hiyo ya Machi 26. Kamanda Satta alisema kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu. Alieleza zaidi kuwa, baada ya kumbaka, watu hao walimdhibiti asipige kelele kwa kumfunga kitambaa mdomoni. “Walipomaliza kumbaka walitokomea kwenye vichaka na kutorokea m

MSHINDI WA SHINDANO LA TEKNOLOJIA KUPATIKANA LEO.

Image
Mshindi wa shindano la uvumbuzi wa Teknolojia mpya itakayo saidia jamii kupatikana leo na kuzawadiwa shilingi milioni tano (5,000,000) katika mkutano wa wadau wa teknologia unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Bites&Bytes ukishirikiana na IBM, TWAWEZA, FSDT pamoja na CBA, mktano huo ambao utahamasisha uendelezaji wa mawazo mapya na uvumbuzi kwa waanzishaji wapya wa biashara na kuwapa mwanya wa kubadilisha mawazo na wadau wengine. Mwanzilishi wa Bits&Bites, Lilian Madeje akiwakalibisha wageni na kufungua mkutano wa Uvumbuzi wa Teknologia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mwalimu Nyerere. Mwakilishi wa IBM na mstakabali wa Innovation, Ben Mann akifafanua jinsi IBM ilivyofanya kazi kwenye Teknologia hapa nchini.  Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes, Zuweina Farah  akizungumza na wadau wa Teknologia waliokusanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar

Rais Magufuli Azungumzia Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi

Image
Rais John Magufuli amewatoa hofu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhusu uteuzi wao kwa kuwataka kuchapa kazi kwa bidii ili wawe na nafasi nzuri ya kuteuliwa badala ya kufanya kazi kwa wasiwasi jambo ambalo matokeo yake yatakuwa kuondolewa. Dk Magufuli alitoa kauli hiyo juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Chato mara baada ya kutua kwa helikopta akitokea Mwanza kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha Rubambangwe kwa mapumziko. Akiwahutubia mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, Dk Magufuli alisema anatambua kuwa bado hajachagua wakuu wa wilaya na wakurugenzi hali ambayo imewafanya baadhi yao kuwa na wasiwasi na kushindwa kutekeleza majukumu inavyotakiwa. “Kama wewe ni mchapakazi mkuu wa wilaya, mkurugenzi una wasiwasi gani? Tena unapokuwa na wasiwasi ndivyo uwezekano wa kung’olewa unakuwa mkubwa,”  alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na kuongeza: “Lazima niwaambie waheshimiwa wakuu wa wilaya, ukiwa na wasiwasi hutafanya kazi na sisi tunakuona tu unaf

Binti Ajinyonga huko Longido ...Aacha majina ya watu anaowadai na Kuagiza Walipe Kabla Maiti Yake Haijasafirishwa

Image
Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge na kuacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote  Amesema amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyewe.Katika ujumbe huo, ametaja majina ya watu anaowadai na kuagiza  walipe madeni yake kabla ya mwili wake kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi. Mimi Jesca Reinald Elisante Leo tarehe 29 , 03 , 2016 nimeamua kujinyonga kwa ridhaa yangu mwenyewe hakuna mtu yeyote anayehusika na kifo changu na hizi ni namba ya Mama  yangu,0672740439. Ninao wadai Mama Diana  33,000/= John Memory card 4 GB Boss Mshahara 60,000/= wanao nidai Zai 20,000/=alipwe na ninao wadai wahakikishe wanalipa kabla sijarudishwa kwetu. NB:HAKUNA ANAYEHUSIKA NA KIFO CHANGU. Ndugu zangu nawapenda sana vitu vyangu vyote vipelekwe kwetu Jau Kwenye Kuni.

MWENYEKITI WA MTAA WA OYSTERBAY, LUBUVA ASAIDIA WATUNZA MAUA WA MBUYUNI JIJINI DAR.

Image
WANAKIKUNDI cha Green Garden ambao wanafanya biashara uuzaji na utunzaji  maua  pembeni kidogo ya kituo cha mabasi cha Mbuyuni jijini Dar es Salaam wapewa mpira kumwagilia maua wa Mita 100 na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva. Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva amesema kuwa ameona vyema kutimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa kwa wanakikundi hicho kwani aliwaahidi kuwasaidi amesema Mwenyekiti huyo wakati wa kukabidhi mpira wa kumwagilia wa mita 100 leo pembeni ya kituo cha mabasi ya Mbuyuni jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo ameashukuru    Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva kwa kutimiza ahadi ahadi yake. "Tulikua na mpira ambao ulikuwa umetoboka tulijitahidi kuziba na makaratasi ili usivuje sasa tumepata mpya tena wa mita 100 sasa tutakuwa kukijitahidi kutunzaji wa mau

Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa Uchaguzi wa Zanzibar

Image
Nchi 10 kati ya 14  za umoja wa Ulaya zimetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania. Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekan i (MCC) kuondoa msaada wa dola 472 ( Trilioni 1 )  wa kufadhili miradi ya maendeleo wakidai kuwa uchaguzi wa Marudio zanzibar haukuwa huru na wa haki. Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada toka mataifa ya nje katika bajeti ya mwaka 2015/2016.  Chanzo:  BBC

WAZIRI WA AFYA AKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MAJIMBO YA MTWARA VIJIJINI, MASASI NA NDANDA

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akiwasili katika hospitali ya Rufaa Ndanda Mission. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari wametembelea Hospitali ya Mji wa Masasi (Mkomaindo), Hospitali ya Rufaa Ndanda Mission na Kituo cha Afya cha Nanguruwe kilichopo Jimbo la Mtwara Vijijini.     Katika ziara hiyo ya siku 2 Mh. Ummy alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kukagua wodi za wagonjwa, maabara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya na wananchi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo hayo. Mh. Ummy alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Dk. John Pombe Magufuli imejikita zaidi katika kuwahudumia wananchi hasa wa kipato cha chini kwa kuimarisha Nidhamu na Uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma. Pamoja na kusimamia Uwazi na matumizi bora ya ra