Posts

Showing posts with the label SIASA

Meya wa Jiji la Arusha Amtaka Mkuu wa Mkoa Amuombe Radhi

Image
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani. "Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma," alisema. Pia, alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu. "Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi...

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu mshahara kwa miezi 10 nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge la bajeti huan...

Ally Kessy: Wabunge Wanaotusumbua Bungeni Wapimwe Madawa ya Kulevya

Image
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara. Keissy alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge. "Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale"  alisema Keissy na kuongeza; "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye ...

Profesa Lipumba Asema Ilikuwa ni MZIGO Mkubwa sana Kumnadi Lowassa......Akanusha Kutumiwa na CCM Kuivuruga CUF

Image
Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa Vyama vya Siasa Prof. Ibrahim Lipumba leo May 4, 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV amesema hakuwa na namba ya Edward Lowassa wakati anajiunga UKAWA. Aidha, kwenye mahojiano hayo Prof. Lipumba amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaiongoza CUF katika kudai haki za wananchi tofauti na Maalim Seif ambaye mara kadhaa ikitokea suala hilo haonekani akisema: “Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi Mkuu tuliingia kwenye maandamano Zanzibar, lakini Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele. Prof. Lipumba amesema pia kuwa Maalim Seif amekuwa akidai kila anapokosana na mtu kisiasa kuwa mtu huyo anatumiwa na CCM akitolea mfano wa Ahmad Rashid, akisema: “Ni kawaida ya Maalim Seif, akikosana na mtu kisiasa anasema anatumiwa na CCM. Rejea mgogoro na Ahmad Rashid". Akizungumzia kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward...

Polepole atolea ufafanuzi mabadiliko ya CCM ili kuondoa uzushi Kuhusu Kumpata Mgombea wa Urais 2020

Image
Mabadiliko ya Katiba ya CCM 2017 yamegusa maeneo gani? Hivi karibuni kumekuwapo maneno ya upotoshwaji juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika tarehe 12 Machi 2017. Napenda kufafanua kwa uchache maeneo ambayo yamefanyiwa Mabadiliko ili kuanzia sasa ieleweke bayana kwamba msingi wa Mabadiliko haya ni Mageuzi Makubwa ambayo yanafanywa na Chama chetu ili kuongeza tija, ufanisi, uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.   Mageuzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanalenga kutizama Uongozi (Leadership), Muundo/Mfumo (Structure/System) na Utawala (administration). Chama chetu kimetimiza miaka 40 mwaka huu (2017) tangu kuanzishwa kwake na kipindi hiki tumeazimia kwa kauli moja kukiimarisha, kukijenga na kukifanya madhubuti. Kazi hii ya Mageuzi ya CCM ilianzishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokaa katika Mkutano wake wa mwenzi Desemba 2016 na baadaye kupitishwa kwa sauti moja na Mkutano Mkuu...

CHADEMA Kuwasha Moto Bungeni

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema matukio yaliyotokea hivi karibuni likiwamo la aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutolewa bastola, yanaweza kubadili upepo wa Bunge linalotarajiwa kuketi siku chache zijazo. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliwaambia hayo waandishi wa habari jana waliotaka kufahamu mipango ya chama hicho katika kutumia mhimili wa Bunge kutokana na uwepo wa matukio ya uvunjaji wa sheria. Katika hilo, Mnyika alisema Watanzania watarajie Bunge lijalo la Bajeti kuwaka moto. “Sisi ndio tunaongoza Kambi Rasmi ya Upinzani na ambacho  ninaweza kuwaambia Watanzania ni kwamba watarajie Bunge la Bajeti kuwaka moto juu ya utendaji wa Serikali. Sasa kuwaka moto namna gani na kuhusu nani ni masuala ambayo yataonekana katika hatua ya baadaye. Naamini safari hii haitakuwa wabunge wa Chadema, Ukawa pekee, naamini Bunge litakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua,”  alisema Mnyika. Chadema Yanunu...

MBUNGE RIDHIWANI NA MADIWANI WA CHALINZE WAIKALIA KOONI CHALIWASA

Image
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (picha na Mwamvua Mwinyi) Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo . Amesema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua. Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba. Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni kubwa hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua. Ridhiwani alifafanua kwamba hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba hayajafukiwa hivyo ni ndoto za alinacha mradi huo kukamilika mwezi huu. Kwa mujibu wake, waziri wa maji anapaswa kulieleza bunge na wananchi wa Chalinze fedha za maji zilizopelekwa kwa ajili ya mradi huo na mwezi wa kuumaliza . "Kama mradi huu utaendelea kusuas...

MBUNGE WA NZEGA HUSSEIN BASHE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIASA YA TANZANIA

Image
Mbunge wa Nzega mjini kupitia CCM Hussein Bashe amepost ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno yaliyosomeka… "Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo "Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu. "Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru. "Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu. "Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu. "Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania ...

LEMA KUFUNGUKA YA MOYONI

Image
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo anatarajiwa kuhutubia wananchi wa jimbo lake katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni mtego kwake, kwani inaweza kumjenga kisiasa ama kumharibia kutokana na kile atakachotamka katika mkutano huo wa hadhara. Lema aliyekaa gerezani kwa zaidi ya miezi minne, aliachiwa kwa dhamana Machi 3 mwaka huu na Jaji Fatuma Maghimbi na wadhamini wawili, waliosaini hati ya dhamana ya thamani ya Sh milioni moja kila mmoja. Gari la matangazo lilikuwa likipita kila kona ya Jiji la Arusha na kutangaza kuwepo kwa mkutano huo na kuhamasisha wananchi wa Jiji la Arusha, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo bila ya kukosa, kwani mbunge huyo ana ujumbe mzito kwa ajili yao. Hata hivyo, si Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Gulugwa wala Lema mwenyewe aliyekuwa tayari kueleza ajenda ya mkutano huo, kwani simu zao za kiganjani zilikuwa zikiita bila ya kupoke...

TUNDU LISSU,MASHA WATAKA KUJUMUISHWA KESI YA KUPINGA UCHAGUZI TLS

Image
Wanasheria wawili wa jijini Dar es Salaam, Tundu Lissu na Lawrence Masha wamesema wataiomba mahakama kuwajumuisha kama wadaiwa katika kesi za kupinga uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walizodai zimefunguliwa jijini Dar es Salaam na Dodoma.  Lissu, ambaye ni mbunge wa Iramba na mwanasheria wa Chadema, na Masha (mwanachama wa Chadema na waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani) wamedai kuwa kesi hizo mbili zimefunguliwa Mahakama Kuu na Godfrey Wasonga mjini Dodoma na Onesmo Mpinzile jijini Dar es Salaam, wakitaka uchaguzi huo uzuiliwe. Mawakili hao wamewahi kupambana katika kesi mbili tofauti zilizohusu vyama vya CCM na Chadema. Wasonga aliwahi kupambana na Lissu katika kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM mjini Dodoma waliopinga ushindi wa mbunge huyo wa Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, wakati Mpinzile alipambana na mwanasheria huyo wa Chadema aliyekuwa akimtetea mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ambaye amehukumi...

MBUNGE LEMA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE IJUMAA

Image
Kwa mara ya kwanza March 10, 2017 Mbunge wa   Arusha Mjini Godbless Lema  Atafanya Mkutano na wananchi wa Arusha akiwa ameambatana na Madiwani  wote Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) wa Mkoani Arusha