Posts

Showing posts with the label MAPENZI NA MAHUSIANO

Akamatwa kwa kumshawishi mpenzi wake ajiue kisha achangishe fedha mtandaoni

Image
Msichana mwenye umri wa miaka 20, Michelle Carter atapandishwa kizimbani Massachusetts nchini Marekani wiki hii akikabiliwa na mashtaka ya kumshawishi mpenzi wake kujiua. Carter anadaiwa kumshawishi kwa njia ya simu mara kadhaa aliyekuwa mpenzi wake, Conrad Roy III aliyefikia uamuzi wa kujiua kwa hewa ya ‘carbon monoxide’ miaka miwili na nusu iliyopita, ambapo mwili wake ulikutwa kwenye gari lake eneo la maegesho ya magari. Upelelezi umeonesha kuwa msichana huyo alikuwa akimtumia jumbe za simu mpenzi wake huyo ambaye awali alimtaka Carter kumshauri baada ya kufanya jaribio ya kujiua bila mafanikio. Jumbe hizo zilimsihi marehemu kujiua tu huku zikimtia moyo kuchukua hatua hiyo. Baada ya Conrad kujiua, mrembo huyo aliingia kwenye mtandao na kuanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kwa lengo la kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiakili akichukulia mfano wa uamuzi wa mpenzi wake huyo, hadi upelelezi ulipomuumbua na kumtia nguvuni. Hata hivyo, mwanasheria wa Boston, Peter Elikann a...

UNAIJUA SABABU YA KUCHUJA KWA PENZI LAKO?

Image
hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja. Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana. Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo. Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi alivyo fundi wa ‘kuyarudi’ ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa. Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kw...

UNAUFAHAMU UMUHIMU WA KUWA NA MWENZA WA MAISHA?

Image
Hivi umewahi kujiuliza kwanini tunakuwa na wenzi wa maisha? Kwanini mapenzi yakawepo? Kwanini wewe una mpenzi na ikitokea mkawa mmehitilafiana unakosa raha? Sina shaka kuwa katika hili, kila mmoja anaweza kuwa na fikra zake mwenyewe, lakini leo nitafafanua sababu za msingi zaidi zinazowafanya wapenzi kuwa pamoja na hatimaye kuishi katika ndoa. Lakini kabla ya kufika mbali zaidi hebu jiulize swali moja, mapenzi humaanisha nini hasa? Kimsingi mapenzi ni hisia za watu wawili ambazo hukutana pamoja zikimaanisha upendo wa dhati. Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja wakahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo. Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi. Wengine hutumia nafasi hii vibaya, baadhi yao huamini kuwa ngono ndiyo mapenzi yenyewe, jambo ambalo halina ukweli. Hebu fuatilia vipengele vifu...

UNAWEZA KUPENDA NA USIPENDWE FANYA UAMUZI SAHIHI

Image
Wakati mwingine unaweza hata kujikuta hujala chochote lakini ukajihisi umeshiba eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa naye karibu tu, yaani yeye kwako ndiyo mambo yote, yeye ndiyo kila kitu kwenye maisha yako! Huo ndiyo utamu wa maisha! Naamini kabisa wapo ambao wako katika aina hiyo ya mapenzi na hao wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuwaweka kwenye mazingira hayo. Lakini sasa wakati wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wengine wanaoishi na wapenzi wao huku mioyo yao ikiwa imesinyaa, yaani hawana furaha kabisa! Kwao kila siku ni karaha na vituko vya makusudi kutoka kwa wapenzi wao licha ya kwamba wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote. Cha ajabu sasa, licha ya baadhi ya watu kutokuwa na furaha katika maisha yao ya kimapenzi eti wanahisi njia sahihi ni kuvumilia huku wakiamini siku moja mambo yatabadilika. Jamani, huenda nikawa na msimamo tofauti kidogo kwani mimi naamini mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzio na kuheshimu ...

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

Image
Kugombana ni sehemu ya maisha ya binadamu. Yawezekana kabisa ulikuwa na mwenzi wako ambaye ulimpenda kwa moyo wako wote na sasa mmeachana. Kutengana kuna mambo mengi, wakati mwingine ilikuwa hasira tu, Siku zote baada ya hasira kuisha, moyo hubaki peke yake katika nafasi yake halisi ya kufanya maamuzi. Hapo ndipo kwenye lengo la mada yetu ya leo. Kwamba kwa msingi huo umegundua kwamba kumbe mpenzi wako uliyeachana naye, bado unampenda. Kwamba hata makosa aliyokuwa akiyafanya, ulimsababishia au si makubwa kiasi cha kuachana na badala yake mnaweza kukaaa na kuzungumza kiutu uzima na kuyamaliza. Yes! Hilo ndilo ninalotaka kulizungumzia, Upo tayari rafiki? Je, uko katika kundi hilo? Unataka kumrudisha mpenzi wako wa zamani? Kama majibu ni ndiyo, mada hii inakuhusu sana. JE, NI SAHIHI? Baadhi ya watu huamini kwamba kurudi kwa mara nyingine kwa mpenzi wa zamani ni kujidhalilisha, kujishusha na kujisalimisha. Kwamba hakuna mwanaume wala mwanamke mwingine yeyote atakayeweza kuwa na...

JINSI JANJAJANJA INAVYOTIBUA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Image
Wengine huwa ni tabia yao ya asili, siyo mkweli kuanzia malezi ya wazazi wake kwani hayasisitizi juu ya ukweli. Ameshazoea kufanya mambo kiujanja ujanja! Kwa mpenzi wa aina hii ni vigumu sana kudumu naye.  Ni mwepesi wa kutamka maneno ya mapenzi lakini ndani ya moyo wake kuna vitu viwili, kwanza anakutamani wewe na pesa zako na wakati huohuo anatamani kuwa na bwana mwingine kwa ajili ya kuongeza kitega uchumi, hili ni tatizo. Mwanamke wa aina hii siyo vigumu kukuita majina mazuri ya kimapenzi lakini akiwa hamaanishi kutoka moyoni mwake kwamba anakupenda, Hawa wapo wengi lakini ni vigumu sana kuwagundua mapema, Hawa huharibu kabisa maana halisi ya mapenzi.  Ngoja nikuulize wewe unayemsaliti mpenzi wako, unavyomfanyia mwenzako hivyo unadhani yeye hana moyo? Hivi hujui kuwa mwenzako anakupenda kwa mapenzi yake yote na amekuchagua wewe uwe mwandani wake? Siku akijiua kwa sababu yako utakuwa katika hali gani? Hebu acha utapeli wako wa mapenzi haraka sana. Kuwa muwaz...

UNAIJUA THAMANI YA ULIYENAYE?

Image
Najua wote tunajua thamani ya mapenzi na pia tunafahamu ni jinsi gani mapenzi yanatesa, yanaumiza na wakati mwingine kuua. Wengi tunafahamu jinsi mapenzi yalivyoleta umoja, undugu na urafiki ambao haukutarajiwa katika maisha yetu lakini kutokana na huyu kuoa yule na yule kuolewa na huyu tumejikuta tukiunganishwa na jambo hilo. Licha ya kujua thamani ya mapenzi na maumivu yake lakini tumeshindwa kuilinda thamani na kuyapuuza maamuzi yake. Tumekuwa wakosaji wakubwa sana kwa wenza wetu tulionao. Tumekuwa hatutambui thamani ya tulionao mpaka pale wanapoondoka mikononi mwetu. Tumekuwa watu tusiothamini mioyo na machozi ya wenza wetu kanakwamba sisi ni wanyama. Kwanini umlize mwanaume aliyekupenda na kukusaidia katika maisha yako? Kwanini umsaliti mwanamke aliyekupa mwili wake na moyo wake pamoja na kukupa thamani kubwa katika maisha yake? Ipi thamani ya machozi yake kwako? Ipi thamani ya mapenzi yake kwako? Kwanini uliache penzi lako lenye furaha na kwenda kwa mtu mwingine ambay...

KABLA YA KUUSIKILIZA MOYO WAKO ZINGATIA HAYA

Image
Kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda. Hayo ndiyo mapenzi jamani! lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje? Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako. Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii. Chunguza Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu...

JIFUNZE KUWEKA MOYONI MAMBO YA NDANI NA MWENZA WAKO

Image
Mtembezi mahaba leo itawaangazia wale ambao wakipewa chakula harakaharaka kesho yake kukimbilia kwa jirani na kumsimulia, utasikia; ‘leo baby wangu amenilisha vijiko vingi hadi nimechoka! Ni fundi wa kulisha kweli tena kwa mikono yote’ sasa unamwambia ili iweje, ina husu? Umeshamuamsha mwenzako, akaamka na kuhamasika sasa akimtamani na yeye akapewa hicho chakula na mumeo utamlaumu nani? Wengine wanafika mbali na kusimulia udhaifu wa mumewe utasikia; ‘Yaani shoga, mume wangu hakuwa hivi, siku hizi anarudi amechoka kweli, ananipa kijiko kimoja tu anadai amechoka’ sawa amechoka, wa kukusaidia kujua kwa nini amechoka ni jirani kweli? Jifunze kutunza siri ya chakula chako na mumeo. Iwe anakulisha kwa mikono yote, iwe anashindwa kukulisha hiyo ni siri yako na yeye. Wengine wao wakikaa kama kusukana au gengeni ama kwenye makundi ya mitandao ya kijamii stori zao kubwa ni kila mmoja kumuelezea mumewe utasikia; ‘Leo usiku sijalala, nimemuandalia vyakula vyote, kala akaniambia hajashi...

MAPENZI YAONESHE KWA VITENDO

Image
Kama ilivyo mambo mengine kuwa na ubunifu ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui. Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha  kwa kufuata haya mambo machache ambayo wanawake wengi huwa wanapenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na kivitendo. 1-Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara. 2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio). 3-Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi. 4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatok...

KABLA YA KURIDHIA KUOLEWA ZINGATIA HAYA

Image
Hakuna mwanamke anayependa kuolewa na mume halafu waachane baada ya muda mfupi, bali kila mwanamke ana kiu ya kutaka kuishi na ampendaye mpaka kifo. Kwa misingi hiyo,ndoa ni jambo muhimu na gumu kwa wakati mwingine hasa linapokuja suala la kuchagua mwenzi wa kuishi naye maishani, hivyo basi mwenye nia ya kuoa utamtambua kwa haya. ALIYE MKWELI Katika hili, hekima na busara nyingi huhitajika kutumika, ngao kubwa ya utambuzi juu ya mpenzi uliyenaye kuwa mume mwema linategemea sana hili. Ukweli ni silaha muhimu sana katika uhusiano. Japo natambua kuwa, kuna wengine watajiuliza utajuaje kama huyu ni mkweli au siyo. Kitendo cha kukutamkia kuwa, anakupenda ni cha ukweli sana hasa kama atakuwa anakupenda kwa dhati, Baadhi ya wanaume wanafikia hatua kuongopa na hata kuazima gari na kujifanya kuwa ni lake ili akunase. Kumbuka wahenga walisema ‘njia ya muongo ni fupi’ hivyo baada ya muda utachambua pumba na nafaka. ANAYEJALI Wahenga waliendelea kunena, `nyota njema huonekana a...

MAUMIVU YA PENZI YANA NGUVU KULIKO CHOCHOTE

Image
Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu. Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia. Inawezekana ni kweli mpenzi wako amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na ninaamini ipo siku utayasahau. Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke, mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi kinavyoikumba ardhi, mara nyingi huwa ni kwa mpito. Kuna msemo ambao hutumika sana katika dunia tuliyonayo usemao ‘hakuna marefu yasiyokuwa na ncha’. Hakika maneno haya yana ukweli fulani ndani yake na ndivyo ilivyo kwamba, mapenzi yanaumiza, yana...

KAMA HUKO TAYARI KWA NDOA ACHA KUFANYA HAYA

Image
Kwa hili hata kidogo halitakiwi kufumbiwa macho, kwa nini wasiojua maana ya ndoa wanawadhalilisha wanawake? Wahenga walilitambua hili zamani, ndiyo maana msichana hakuweza kuolewa mpaka apitie mafunzo ya kujitambua yeye ni nani ndani nyumba. Kweli asiye na hamu hawezi kuiona tamu, Jamani kuolewa si mchezo wa kuigiza bali ni maisha yanayotambulika kihalali. Unatakiwa kutambua kwamba ndoa ina raha yake hasa ukiijua, mumeo utamuona mfalme na wewe utakuwa malkia. Leo hii mtu anaolewa, hakai na mumewe zaidi ya kuzunguka kila kona, anakuwa kiguu na njia. Inaoneka wazi hiyo ndoa yako umeolewa ili uonekane nawe umeolewa, lakini huna hamu nayo, siku zote kwako huioni tamu kwa sababu huna hamu nayo. Mwenye kuwa na hamu na ndoa hawezi kukaa mbali na mumewe, wala kujichukulia madaraka mkononi, bali huikumbatia ndoa yake kwani hiyo ndiyo pingu ya maisha yake, kama hujawa na hamu na ndoa usiolewe. Hakuna tamu bila kuwa na hamu.

LINDA PENZI LAKO KWA NAMNA HII…!!

Image
Kuna sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako, uishi na mke au mume si kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria. Hivi ni vipengele baadhi tu, wanandoa na wapenzi wanapaswa kuvitambua. Kwanza kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi si lazima ufanye tendo la ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili. * UPENDO KUTOKA KWA YULE UMPENDAE. hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi, hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati yeye hana habari na wewe. * AMANI. Watu wengi wana wanaume na wanawake warembo, lakini hawafurahii mapenzi...

HUKATAZWI KUFANYA ILA PUNGUZA KASI…!

Image
Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi wamehemkwa na miili yako. Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu. Ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahi. KUPOTEZA HAMU YA TENDO Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara. KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili u...

JINSI YA KUWEKA MIPAKA NA MAMA MKWE

Image
Kila binti ambaye anatarajia kuolewa au ambaye ameolewa mara nyingi likitajwa neno  “ Mama Mkwe ”  hupata mshituko kidogo hasa jamii zetu za kiafrika ambazo bado mtoto wa kiume mara nyingi humsikiliza sana mama yake katika maamuzi mengi ya kwenye ndoa yake kuliko mke wake anayeishi naye, Wanawake wengi walio katika ndoa mpya hupata wakati mgumu sana pale wanapoona mama mkwe anakuwa na uwezo wa  kum-control   mume wake na matokeo yake utani wa jadi unaanza ( vita ) kati ya mama mkwe na binti na wakati mwingine huleta mvurugano mkubwa kabisa wa ndoa. Kila mafanikio huwa na siri basi hata kuishi vizuri na mama mkwe kuna siri zake muhimu ambazo ni kama ifuatavyo. UPENDO Mama mkwe ni mama ambaye bila yeye huyo mume uliyenaye usingempata, hata kama ungeolewa na mwanamke mwingine bado hata huko ungepata mama mkwe ingawa asingekuwa yeye, Na pia kama unahitaji mahusiano bora na familia imara basi mahusino mazuri na mama mkwe ni muhimu sana, Hata k...

MAMBO SITA YA KUZINGATIA ILI UISHI VIZURI NA MKWE WAKO

Image
Maranyingi imekuwa ni tatizo kwa mtu na mkwe wake (hasa mke na mama mkwe) kuishi kwa umoja na upendo. Utakuta mama anaona ni vigumu kuacha mtoto wake wa kiume apangiwe mambo yake na mtu mwingine(mkewe) na mke naye anaona tabu kuchanganyika na familia ya mume. Tatizo hili linaweza kuwa kubwa hata kuhatarisha ndoa na familia. Uelewano na hekima inahitajika sana kutatua matatizo haya. Hapa nimefafanua baadhi ya mambo machache yanayoweza kukusaidia kuboresha mahusiano yenu. 1. Onyesha upendo kwa vitendo Usiruhusu kuongozwa na hisia zako, bali umruhusu Mungu akuongoze ili uweze kutenda kwa upendo. Haijalishi unajisikia vipi, chagua kutenda matendo ya upendo kwa mkwe wako (mama au mtoto). Amini kwamba unapoonyesha upendo Mungu atakufungua moyo wako na kukuwezesha kujisikia vyema. 2. Uwe mvumilivu Usiwe na mategemeo makubwa kuwa siku ya kwanza tu kuonana basi mtapendana na kuwa na mahusiano ya karibu. Jipe mda na pia mpe na yeye muda kwa kuishi kwa kuvumiliana na hatimaye ma...

UNAYAJUA MAUMIVU YA MAPENZI?

Image
       Hakuna mwenye moyo ambaye anafurahishwa na maumivu katika mapenzi. Hapa nazungumzia usaliti, unyanyasaji, masimango na mengine mengi katika uhusiano wa kimapenzi. Wapo watu ambao ni wa kwanza kuwaumiza wenzao lakini wao wakiumizwa ni matatizo tupu! Wanajihisi kama wao pekee ndiyo wenye moyo wa kuumia lakini wenzao hawapati maumivu. Hivi hii inaingia akilini kweli? Siku zote lazima ufahamu kwamba mioyo yote ina nyama. Kuna mambo mengi ambayo mpenzi akifanyiwa na mwenzake lazima ataumia sana. Ingawa kuna mengine yanafichwa au kupasishwa kama sahihi, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba yanaumiza. Kikubwa ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba maumivu hayo yapo sawa kwa kila mmoja. Haijalishi jinsia, umri, kabila wala dini, maumivu ya mapenzi yote yanafanana. Kufanana huko kunasababishwa na mioyo yote kuwa na nyama! Kwa sababu mioyo yote ina nyama basi unatakiwa kufahamu kwamba, jinsi unavyoumia wewe moyoni mwako, ndivyo mpenzi wako anavyoumia...