WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU UFARANSA
Waziri wa mambo ya ndani ufaransa bwana Bruno Le Roux amejiuzulu kufuatia kuibuka shutuma juu nyake kuwa aliwatafutia mabinti wake wawili kazi katika bunge wakati wakiwa wanafunzi Inasemekana alfanya hvyo kati ya mwaka 2009 na 2016 .Waendesha mashtaka walifanya uchunguzi wa awali kuhusu mikataba yenye thamani ya karibu dola elfu sitini ambazo bwana Le Roux aliwapa binti zake Amesema hakuna sheria ya bunge iliyokiukwa na watoto wake walifanya kazi kwa uhalali, lakini hakutaka kuwa kikwazo kwa Serikali Bwana Roux amekua waziri wa mambo ya ndani tokea 6 December 2016 mpaka 21 march 2017