Posts

Showing posts with the label BURUDANI

Hussein Machozi Asimulia Alivyofumaniwa na Mke wa Mtu na Kisha Kupewa Kichapo Nchini Kenya

Image
Msanii Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake. Hussein Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel. "Kwa hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao. "Wakatuzunguka pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na kukimbia.  "Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa m...

RAHA ZA PWANI YAFANYIKA DMV

Image
 Bi. Grace Mgaza Sebo akiongoza mchezo wa bahati nasibu iliyofanyika leo Ijuamaa kwenye tamasha la Raha za Pwani iliyofanyika katika hoteli ya Hampton Inn College Park, Maryland  na kuhudhuriwa na wadau wa miziki hiyo wakiongozwa na Dj Moe. Picha na Vijimambo na Kwanza Production.  Mtoto Aaliyah akichanganya tiketi za bahati nasibu kusudi ya kutangazwa mshindi.  Mtoto Allan akijiandaa kumtangaza mshindi wa kwanza aliyeamka na bahati usiku huo wa Raha za Pwani.  Rose Millinga (kushoto) akiibuka mshindi wa kwanza akikumbatiana na Bi. Grace Mgaza Sebo moja ya waandaji wa tamasha la Raha za Pwani iliyofanyika siku ya Ijumaa March 31, 2017 katika hotel ya Hampton Inn College Park, Maryland nchini Marekani.  Rose Millinga akiwa na zawadi yake katika picha ya pamoja na waandaji wa tamasha la Raha za Pwani  kushoto ni Bi. Grace Mgaza Sebo na kulia ni Steven Mgaza. Wapili toka kushoto ni mtoto Aaliyah. Mratibu wa Raha za Pawani Bw. Steven...

Mahakama Yamuonya Agness Masogange

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange baada ya kutohudhuria kesi hiyo mahakamani. Kesi hiyo ambayo imetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu mkazi wa Kisutu Wilbard Mashauri wakili wa serikali Adolf Mkini amesema kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepham. Ameeleza kuwa mshitakiwa anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam  alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine) na kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam. Mshitakiwa anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015 na kuwa uopelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika licha ya mshtakiwa kutokuwepo mahakamani hapo. Hata hivyo  wakili wa Masogange, Nictogen Itege aliwa...

Sakata la Madawa: Vanessa Mdee Akamatwa na Polisi, Apelekwa kwa Mkemia Mkuu

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Akizunguzumzia taarifa hiyo, Mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Amin Tenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Vanessa alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitaja majina ya watuhumiwa wa dawa hizo mapema mwezi uliopita. Vanessa ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya, lakini hakuweza kuripoti kwa wakati sababu alikuwa nchini Afrika Kusini kikazi. Baada ya kujisalimisha, Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo na kama walikuta ushahidi wowote nyumbani kwa mwanamuziki huyo.

Saida Karoli Asimulia Alivyoporwa Haki Zake Katika Muziki Kisa Kutojua Kusoma na Kuandika

Image
Jana kupitia kipindi cha Take One  cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi  alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili  Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana  haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na a ka dai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo. Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia  ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea. ”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure ”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja ...

TAZAMA PICHA:ALLY KIBA APOKEWA KISHUJAA, NI BAADA YA KURUDI NA TUZO YA MSANII BORA WA KIUME AFRIKA

Image
 Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika                  Mashabiki wa AlyKiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani  Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake  Aly Kiba akiwa na Meneja wake  Seven Mosha mara baa da ya kuingia katika gari hiyo maaalum  Ally Kiba akiwa katika mitaa ya Kariakoo huku akiwa amezunguskwa na mashabiki mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona Tunzo yake ya Mtv base kama msanii bora wa kiume Afrika  Mashab...

TID: NINGEKUA TAJIRI KAMA NISINGEKUA MTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

Image
Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la  TID, amekiri kuwa kujihusisha kwenye utumiaji wa dawa za kulevya kumemrudisha nyuma kiuchumi. Akiongea kwenye kipindi cha XXL, kupitia Clouds FM Ijumaa hii, Mnyama ambaye alikiri hadharani kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya dawa hizo, alisema hadi sasa angekuwa na utajiri wa kushangaza. Anasema dawa hizo zina gharama kubwa. “Nadhani ningekuwa nimenunua kama magari mengine manane, ningekuwa nimefanya video za muziki kadhaa zenye kiwango kikubwa. Lakini nilitumia hela nyingi sana hasa pale ninapoenda kujirusha ningetumia hela nyingi sana, Lakini hii imefikia mwishoni, "alisema TID. Staa huyo amedai kuwa dawa zilimfanya awe na mtazamo tofauti katika vitu vingi ambavyo alivichukulia rahisi rahisi. “When you are high you think you are on top, nobody can touch you sababu you are under influence unaanza kugombana na watu, ukawajibu watu vibaya, but when you are clean unaweza ukafanya vitu, you can save a lot of ...

VIDEO:USIPITWE NA KICHUPA KIPYA CHA DIAMOND FT NE-YO-MARRY YOU

Image
Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, video ya Diamond Platnumz ya wimbo wake, Marry You aliomshirikisha Ne-Yo imetoka. Kwa mara ya kwanza video hii imewekwa kwenye channel ya Vevo  ya staa huyo.  

UNIVERSAL MUSIC GROUP(UMG) YATANGAZA RASMI KUMSAINISHA DIAMOND

Image
Hatimaye record label kubwa duniani, Universal Music Group (UMG), imemtangaza rasmi kumsainisha Diamond Platnumz. Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo. Wimbo wake,  Marry You  akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza  kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music. “He’s a star, he is talented and full of energy and creatively he’s on par with any international artist I’ve worked with,”  anasema Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Dlamini. “He’s focused and determined to succeed. He’s passionate about his country, his people , his language and his culture and I love that. He is a first class performer on stage, his new material is authentic, fresh and African, yet it will touch people across the globe. Artists like him are the reason we do what we do.”

USIPITWE NA VIBONZO VILIVYOBAMBA LEO MTANDAONI

Image

UMEISIKIA HII,HARMORAPA AJIBU MAPIGO BAADA YA MOSES IYOBO KUMUITA NYANI

Image
Baada ya Mtangazaji wa XXL ya Clouds FM, B Dozen kupost picha Instagram akiwa na mtafiti wa wanyama aina ya Sokwe, dancer wa Diamond Platnumz Mose Iyobo alicomment kwenye picha hiyo kuwa mtafiti huyo aje na Dar es salaam kumfanyia utafiti Harmorapa. Leo  January 30 2017 kupitia YOU HEARD ya XXL clouds FM, Soudy Brown ameongea na kuhusu  issue ya  Mose Iyobo kumfanisha Harmorapa na Nyani ambapo haya ni majibu ya Harmorapa baada ya hiyo comment. "Asante sana Mose kwa kuniita nyani ila akae atambue anamkufuru Mungu kwa sababu ndio aliyeniumba kwa hiyo anavyonifananisha na nyani na mimi nafananishwa na Harmonize pia na Hamornize ni nyani kwa hiyo tuko nyani wawili." amorapa Mose Iyobo kwa upande wake amesema: "Mimi sioni cha ajabu, kuna mtu anaitwa Simba na anafurahi, kuna mtu anajiita Dudu baya na anafurahi leo mtu kumuita mtu nyani yanakuja maneno mengi, wao wanatukana maneno mangapi na hujasikia nimeenda kusema sehemu" ==>Wasikilize Hapo Chini ...

WASTARA AWEKA WAZI SABABU YA KUACHA WANAUME

Image
Msanii wa filamu, Wastara Juma ameweka wazi sababu kubwa ambayo ilimpelekea kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Bondi Bin Salim na kwenda kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kisha kuachana naye na kurudiana tena na mpenzi wake  Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha (EATV) Wastara anasema aliamua kuachana na Bond kutokana na tabia yake ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi na pombe pamoja na tabia zingine ambazo yeye alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana naye. "Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpka Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi, mpka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi, kwanza kwenye mahusiano kulikua hakuna uaminifu kabisa, ilifikia hatua mpka kuna watoto wengi sana walikuwa wanaletwa wengine ni kw...

Harmo Rapa Ang'ang'ania Jina la Harmonize ,Atoa Sababu Hizi Nzito za Kufanya Hivyo..!!!

Image
Msanii wa bongo flava ambaye ndiyo anaanza kuchipukia, Harmo Rapa, amesema kuwa hana mpango na wala hawezi kubadili jina hilo lililompa umaarufu kwenye muziki kwa hofu ya kupoteza mashabiki wake.  Msanii huyo anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'USIGAWE PASI'. ametoa msimamo huo kupitia eNewz ya EATV iliyomtafuta kuzungumza naye kuhusu mpango wa kubadili jina lake na kutotumia jina la 'Harmo Rapa'. “Mimi sina mpango wa kubadili jina langu kwa sababu naogopa kupoteza mashabiki zangu na ukiangalia kwa sasa jina la Harmo Rapa limeshakuwa kubwa na tayari nimeshajitengenezea mashabiki kupitia jina hilo” Pia amesema kuwa hana mpango wa kwenda WCB na wala hahitaji msaada wowote kutoka kwao huku akionesha jeuri kuwa angeweza kutoka hata bila kutumia jina hilo. "Hata bila kufananishwa na Harmonize mimi ningetoka tu" Harmo Rapa ni moja kati ya wasanii ambao wamepata kiki ya kutosha kutokana tu na muonekano wake ambapo watu wengi wamekuwa ...

Katuni 6 Nzito Zinazosumbua Leo:SIASA, MICHEZO & ELIMU

Image