Posts

Showing posts with the label TANZIA

Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku). Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua. Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana  saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

Lowassa, Sumaye, Mabata Watema Cheche Msibani

Image
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki ya kisiasa.  Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia.  “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure." Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “ Hata njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu  ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.” ...

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA BLOGGER NA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR

Image
Pichani ni Mpendwa wetu Jennifer Livigha maarufu aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la CHINGA ONE  na Mwanachama mwanzilishi wa  Tanzania Bloggers Network  (TBN) enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake Kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.  Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer  Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama  Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer  Baadhi ya wanachama wa...

GOLIKIPA DAVID BURHAN WA KAGERA SUGAR AFARIKI DUNIA

Image
Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za bongo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo. "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani" Marehemu David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es Salaam, Abdallah Buruhan.

RAIS WA ZAMANI WA IRAN AKBAR HASHEMI RAFSANJANI AFARIKI

Image
Akbar Hashemi Rafsanjani Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salamu za rambirambi za kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Akbar Hashemi Rafsanjani, aliyefariki dunia, akiwa na umri wa miaka themanini na mbili. Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji. Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa. Siku tatu za maombolezi zimetangazwa. Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran. BBC

HATIMAYE MAREHEMU SITTA APUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yake yaliyofanyika jana Urambo mkoani Tabora  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu. Anayefuatia ni Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

KWAHERI HAFIDH SOKA LA TANZANIA LITAKUKUMBUKA

Image
Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar na mwamuzi wa zamani wa soka nchini Hafidh Ali Tahir amefariki dunia alfajiri ya leo kwenye Hospitali ya General mjini Dodoma ambapo alikuwa amelazwa akipata matibabu. Moja ya waamuzi bora wa soka nchini kuwahi kutokea hatimaye ameondoka. Umahiri wake katika kuchezesha Kandanda ni moja ya vitu vilivyomjengea heshima kiasi cha wananchi wa jimbo la Dimani, Zanzibar kumwamini na kumteua kuwa Mbunge wao. Hafidh amewahi kuwa mwamuzi wa FIFA na ni moja ya waamuzi wachache kutoka Tanzania waliopata nafasi ya kuchezesha michuano ya kimataifa kama vile Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 16 mwaka 1989 kabla ya kustaafu mwaka 1994. Marehemu alikuwa mwanachama wa Yanga na amefariki masaa machache kabla ya kuanza kutumikia cheo chake kipya cha  Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge wana Yanga mjini Dodoma ambapo alichaguliwa siku ya jana akiwa chini ya Menyekiti Venance Mwamoto. Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa M...