MAAZIMIO NA MAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LILILOKUTANA KWENYE MAKAO MAKUU YA CHAMA, MJINI ZANZIBAR TAREHE 27 SEPTEMBA, 2016 Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) limekutana leo, Jumanne, tarehe 27 Septemba, 2016 katika kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya Chama, mjini Zanzibar na ambacho kiliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 80 (1). Wajumbe 43 kati ya wajumbe 53 wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa walihudhuria kikao hicho. Agenda tatu zilizotayarishwa na kuwasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa zilijadiliwa na kufanyiwa maamuzi ambazo ni: 1. Kujadili barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya tarehe 23/09/2016; 2. Kupokea na kujadili mashtaka dhidi ya Prof. Ibrahim Lipumba kutokana na hujuma alizozifanya tarehe 24/09/2016 Afisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam; 3. Kumjadili na Kumhoji Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya kikao n...