JE WAJUA KIFAFA KINASABABISHWA NA MATUMIZI MABAYA YA DAWA
Karibuni tena wapenzi wasomaji katika makala hii ya afya yako leo tutaangalia ugonjwa kifafa kwa kutazama dalili za awali,vigezo hatarishi,uchunguzi uambatanao na ugonjwa wa kifafa na hatua za kuchukua iwapo mtu amepatwa na kifafa. Ubongo wa binadamu umeundwa na zaidi ya seli za neva (seli za fahamu) bilioni mia moja.Seli hizi zote huwasiliana ambapo baadhi huzichokoza nyingine kutuma jumbe zaidi wakati nyingine huzifanya nyingine kutotuma ujumbe kama inavyotakiwa.Utendaji mzuri wa ubongo unategemea uwiano katika kutuma ujumbe.Utumaji usio na udhibiti hupelekea mlipuko wa umeme katika seli za ubongo ambapo huweza kupelekea mtu kupata kifafa (seizure) hali ambayo huambatana na kupoteza fahamu,kuzubaa,kukakamaa misuli,kuchanganyikiwa au kuchezesha viungo haswa mikono na miguu. Sote tuko katika hatari ya kupata kifafa.Kifafa chaweza tokea bila sababu dhahiri lakini watu waliowahi kudhurika ubongo wako katika nafasi kubwa ya kupata kifafa. Kifafa hakirithiwi ingawa mara chache hutokea h...