MAAJABU YA SAMAKI NA UZAZI WAKE

Kumbe tabia ya binadamu  kupenda vizuri imeshamiri hadi kwa wanyama, kinadada siku hizi utasikia wakisema wahanitaji wanaume wazuri ‘handsome’ wenye pesa na kila aina ya mvuto; hili halikuishia huku tu kumbe hata viumbe na wanyama nao wana sifa ya kuchagua madume mazuri ya kuzaa nayo.

Utafiti umebaini samaki jike anakawaida ya kuchagua samaki dume wazuri na kuzaa nao watoto wenye jeni nzuri ingawa jambo hili si rahisi kwani changamoto iliyopo ni kwamba  mayai yao yanaungana na mbegu za samaki dume zilizopo majini, hivyo ugumu uliopo hapa ni samaki jike kushindwa kuzuia mayai yasiungane na mbegu  za madume wabaya.

samaki

Hivyo nini kinatokea? Mwanabiolojia Suzanne Alonzo kutoka Chuo Kikuu cha Yale na wenzake wametafiti samaki aina ya ocellated wrasse na kugundua kuwa majike wana uwezo wa kuchagua kuzaa watoto wenye jeni nzuri.

Samaki dume wana sura na tabia tofauti, baadhi yao ni wakubwa wenye rangi ya kupendeza, wanajenga viota kwa mwani na kuyalinda mayai kwa makini, lakini wengine ni wadogo na wavivu, hawawachumbii majike wala kuyalinda mayai. Bila shaka majike wote wanapenda kuzaa watoto na wale wanaofanya bidii. Lakini wale wavivu ni wajanja, wanakwenda kwenye viota vya wengine bila mwaliko. Jambo baya zaidi ni kwamba idadi ya mbegu za uzazi za kiume za wale wavivu ni milioni 4, lakini za wale wenye bidii ni milioni 1 tu.

mayai-ya-samaki

Hivyo bila shaka madume wavivu watashinda, lakini matokeo ni tofauti kwani utafiti umebaini theluthi mbili ya mayai yataungana na mbegu za uzazi za kiume za madume wazuri; kinachotokea ili samaki jike waweze kutimiza adhma yao ni kuamua kuyafunika mayai yao kwa majimaji ya ovari. Mbegu za uzazi za kiume za madume wazuri zina uwezo mkubwa wa kupita majimaji hayo na kufikia mayai kwa kasi zaidi, hivyo ingawa majike hawawezi kuwazuia madume wavuvi wasije, lakini bado wanaweza kuchagua baba wazuri kwa watoto wao.

Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!