Posts

Showing posts with the label MICHEZO

SAMATTA ATUPIA MBILI KRC GENK IKIITANDIKA KAA GENT 5-2 EUROPA LEAGUE

Image
Mshambuliaji nyota Mtanzania,  Mbwana Samatta  ameonyesha kweli ni moto baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ikishinda kwa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Gent. Genk imeichapa Gent, zote za Ubelgiji kwa mabao 5-2 katika mechi ya raundi ya 16 Bora Europa Cup, kuwania kwenda robo fainali. Samatta ambaye watangazaji wengi wa runinga barani Ulaya wamekuwa wakitamka jina lake “Bwana Samatta”, alianza kufunga katika dakika ya dakika ya 41, likiwa bao la tatu. Kabla Ruslan Malinovsky alikuwa amefunga bao kwa mkwaju wa adhabu katika dakika ya 21 na Gent wakasawaisha kupitia kinda Mnigeria, Samuel Kalu katika dakika ya 27. Omar Colley raia wa Gambia akaongeza bao la pili dakika ya 33 kabla ya Samatta kufunga na Jere Uronen akafunga la nne kabla ya kwenda mapumziko. Gent ambao walikuwa nyumbani walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 61 kupitia Kalifa Coulibaly. Wakati Gent wanaona mambo yanaenda vizuri...

UCHUMI WASABABISHA YANGA KUACHANA NA HAS PLUIJM

Image
Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Yanga, yamesababisha timu hiyo kuachana na mkurugenzi wake wa ufundi, Hans Pluijm. , Pluijm amethibitisha kupokea barua kutoka kwa uongozi wa timu hiyo ambao umeamua kuachana naye ili kupunguza gharama. “Ni kweli nimepokea barua kutoka kwa uongozi ya kutoendelea kuhitaji huduma yangu kutokana na matatizo ya kifedha yayonaikabili klabu hiyo kwa sasa,” alisema Pluijm. Aliongeza, “Kuhusu mipango iliyo mbele yangu siwezi kuiweka wazi kwa sasa ila nitawafahamisha nini kitafuata ndani ya muda mfupi ujao. Ninawashukuru kwa ushirikiano mkubwa nilioonyeshwa kwa siku zote nilizokuwepo hapa.” Alipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliomba atafutwe baadaye kwani alikuwa kikaoni.

WAZIRI NAPE MGENI RASIMI FAINALI ZA ULEGA CUP ZITAKAZOFANYIKA MACHI 5 MKURANGA

Image
Timu ya kata ya Tengelea, Tengelea FC  imefunzu kuingia katika fainali ya Ulega Cap baada ya kuifunga Timu ya Mwandege FC  bao 1 – 0 katika mcheezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana . Bao la timu ya Tengelea lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia mchezaji  wao Andew Joseph aliyepokea cross ambayo ndio ilipa ushindi timu hiyo. Timu ya kata ya Tengelea, itaingia fainali kwa kukipiga na timu ya Kisiju na mechi itanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Mwandege FC na Lukanga FC. Mgeni rasmi katika fainali za Ulega CUP ni Waziri Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye. Akizungumza na waandishi wa habari muandaji wa mashindano hayo Mbunge wa  Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa mashindano yameibua vipaji ya vipya. Amesema kuwa inahitaji uwekezaji katika michezo kutokana na vijana kuonyesha vipaji vyao ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wacheza...

SIMBA YAITANDIKA YANGA MABAO 2 KWA 1

Image
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga. Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo. Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi, huku wakijaribu Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo a...

SIMBA HAO ZANZIBAR, WAENDA KUCHUKUA MAKALI YA KUIA YANGA FEBRUARI 25

Image
Wachezaji wa Simba wakiingia eneo la bandari kwenda kupanda boti ikiwa ni safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo akiwa anaongoza kuelekea eneo la kusubiria boti wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.    Wachezaji wa Simba wakiwa wanasubiri kukaguliwa tiketi getini wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.  Wachezaji wa Simba wakiwa wanasubiri kukaguliwa tiketi getini wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.  Kocha wa Simba Joseph Omog akiongea na shabiki wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa safari ya Zanzibar kw...

NSSF YAFIKA NUSU FAINALI YA MASHINDANO YA SOKA YA MASHIRIKA YA UMMA

Image
Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee  akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tanesco wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya michuano ya Ligi ya Mashirika ya Umma uliofanyika kwenye uwanja wa TPDC Mikocheni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Tanesco ilishinda 4-1. (Picha na Francis Dande). Wachezaji wa NSSF wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wao na Tanesco. Wachezaji wa NSSF wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya mchezo. Viongozi wa NSSF pamoja na wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja. Timu za NSSF na Tanesco zikikaguliwa. Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee akijaribu kuokoa  moja ya hatari langoni mwake. Nahodha wa NSSF, Baome Kiwamba akimiliki mpira. Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Shaban Enzi akichuana na beki wa Tanesco, Nicholous Peter katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya timu zaMashirika ya Umma. Kiungo wa NSSF, Salum Swedi akichuana na Fortunatus Mgumba. Mshambuliaji wa NSSF, Baome Kiwamba akichuana na beki wa Tanesco, Stanley U...

ARSENAL YAFANYA MAUWAJI KOMBE LA FA, YAWAPIGA 5-0 SOUTHAMPTON

Image
Danny Welbeck akishangilia baada ya kufunga mabao mawili dakika za 15 na 22 katika ushindi wa 5-0 wa Arsenal dhidi ya wenyeji Southampton leo Uwanja wa   St Mary's kwenye mchezo wa Raundi ya Nne Komb la FA England. Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa  na Theo   Walcott dakika za 35, 69 na 84 

BOSSOU AREJEA KUONGEZA NGUVU YANGA

Image
YANGA SC imesema inamtarajia beki wake tegemeo, Vincent Bossou kurejea nchini kuanzia kesho baada ya kukosekana mwezi wote huu akiwa na timu yake ya taifa, Togo kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba wanatarajia Bossou atawasili wakati wowote kuanzia Jumapili baada ya Togo kutolewa AFCON. “Kwa kweli matarajio yetu atakuwa hapa kuanzia Jumapili, kwa sababu kule timu yake imetolewa na anafahamu anatakiwa kurejea hapa haraka kuendelea na majukumu yake,”aliseam Baraka. Vincent Bossou anatarajiwa kurejea nchini kuanzia kesho baada ya Togo kutolewa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Gabon Bossou alikuwa nchini Gabon kwenye AFCON, ambako kwa bahati mbaya timu yake, Togo imetolewa baada ya hatua ya makundi tu kufuatia kuambulia pointi moja tu baada ya mechi za tatu za Kundi A. Ilifungwa 3-1 mara mbili na Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutoa sare ya 0-0 na Ivory ...

AZAM YAICHAPA SIMBA TENA 1-0, SAFARI HII NI BOCCO

Image
Bao pekee la Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bocco alifunga bao hilo dakika ya 70 baada ya kupara mpira mrefu wa mshambuliaji Mghana Mohammed Yahya na kumhadaa beki kisiki wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali kabla ya kumchambua kipa Mghana, Daniel Agyei.  Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo ndani ya mwezi mmoja Simba wanapewa na Azam, baada ya Januari 13 kufungwa pia 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar, bao pekee la Himid Mao.  John Bocco (kulia) akimlamba chenga beki wa Simba, Method Mwanjali leo Kipa wa Azam, Aishi Manula akidaka mpira dhidi ya kiungo wa Simba, Jamal Mnyate huku mchezaji mwenzake, Joseph Mahundi akiwa tayari kusaidia Kiungo wa Simba, Muzamil Yassin akipasua katikati ya wachezaji wa Azam, Joseph Mahundi (kushoto) na Frank Domayo (kulia) Mshambuliaji wa Si...

VIJANA ASPIRE KWENDA SENEGAL, VIPAJI VINGINE VYATAFUTWA

Image
Vijana watatu wa Tanzania ambao vipaji vyao vilitafutwa katika Mradi wa Aspire, wanatarajiwa kuondoka kesho Januari 5, 2017 kwenda Dakar, Senegal kwa ajili ya kujijunga na Akademi ya Aspire kuendelezwa kwa miaka mitano ijayo. Vijana hao ni Ally Hamis wa Kituo cha Makongo, Dar es Salaam ambaye alizaliwa Septemba 16, 2003; Baraka Kadety wa Mzumbe, Morogoro aliyezaliwa Machi 11, 2003 na Martin Gabriel aliyezaliwa Julai 17, 2003 kutoka kituo cha Tabata, Dar es Salaam. Vijana hao walitafutwa mwaka jana katika vituo 14 za Aspire vilivyoko hapa nchini. Vituo hivyo viko mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Arusha na Kilimanjaro. Mradi wa Aspire unaoendeshwa kwa ushirikiano wa Makao Makuu yalioko Qatar na Klabu ya Barcelona ya Hispania una lengo la kutafuta vipaji na kuvikuza katika vituo vyao. Kwa Bara la Afrika wana kituo Senegal (Dakar) wakati Makao Makuu yako Doha, Qatar. Wakiwa Dakar, Senegal vijana hao wataendelezwa vipaji vyao pamoja na masomo na kwa kufanya kwao vema, w...

MASHARTI LIGI KUU YA VODACOM DURU LA PILI

Image
Duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza leo Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu. Katika mechi za Leo, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru. Michezo mingine ya leo ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex. Jumapili, Desemba 18, m...