ULALAPO FANYA HAYA KUEPUKA KUKOROMA

Kama kuna kitu kinachokera kupita maelezo ni pale inapotikea unalala na mtu anayekoroma. Khaaaaaa! Inakera kweli kweli kwani kelele za mtu anayekoroma hukosesha wengine kufaidi raha ya usingizi kwa sababu ukweli ni kwamba ukiachilia mbali raha ya kujinyoosha pia usingizi una raha yake asikwambie mtu; basi inapotokea mtu akakukatisha raha hiyo huwa tafrani tupu.

kukoroma

Watu wengi wana tabia ya kukoroma wanapolala, lakini kukoroma siyo kuzuri sana kwani familia yako pengine hushindwa kupata usingizi vizuri kutokana na makelele yanayotokana na kukoroma kwani maana halisi ya kukoroma kunamaanisha kuwa pumzi zako haziko sawa, wataalamu wa masuala ya afya wanasema wakati mtu anapokoroma kunaweza kusababisha kukosa pumzi na kupelekea kifo. Kwa hivyo, zifuatazo ni ‘tips’ kadhaa zitakazokusaidia kubadilisha hali hii.

Kwanza kuchagua mito laini inayoweza kufanya shingo yako iwe vizuri, ambayo itakusaidia kupumua vizuri.

kukoroma

Pili tumia mashine ya (humidifier) ili hewa ndani ya chumba iwe ya unyevu na kukusaidia koo lako kutokuwa kavu.

Tatu, kunywa asali kidogo kulainisha koo lako na usinywe pombe kwani inapandisha shinikizo la damu na kuwa juu hivyo kusababisha  koo lako kubana na kuzuia kupata pumzi.

kukoroma

Nne, ambalo ndilo jambo la msingi kabisa linalosisitizwa na wataalamu wa afya ni kufanya mazoezi mara kwa mara ! Mazoezi ni dawa iliyothibitika kutibu magonjwa mengi.

Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!