RAIS WA ZAMANI WA IRAN AKBAR HASHEMI RAFSANJANI AFARIKI

Akbar Hashemi Rafsanjani
Akbar Hashemi Rafsanjani
Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salamu za rambirambi za kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Akbar Hashemi Rafsanjani, aliyefariki dunia, akiwa na umri wa miaka themanini na mbili.
Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji.
Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.
Siku tatu za maombolezi zimetangazwa.
Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran.BBC

Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!