KAMA HUKO TAYARI KWA NDOA ACHA KUFANYA HAYA

Kwa hili hata kidogo halitakiwi kufumbiwa macho, kwa nini wasiojua maana ya ndoa wanawadhalilisha wanawake?

Wahenga walilitambua hili zamani, ndiyo maana msichana hakuweza kuolewa mpaka apitie mafunzo ya kujitambua yeye ni nani ndani nyumba.

black-couplesnn

Kweli asiye na hamu hawezi kuiona tamu, Jamani kuolewa si mchezo wa kuigiza bali ni maisha yanayotambulika kihalali.

Unatakiwa kutambua kwamba ndoa ina raha yake hasa ukiijua, mumeo utamuona mfalme na wewe utakuwa malkia. Leo hii mtu anaolewa, hakai na mumewe zaidi ya kuzunguka kila kona, anakuwa kiguu na njia.

black-oo

Inaoneka wazi hiyo ndoa yako umeolewa ili uonekane nawe umeolewa, lakini huna hamu nayo, siku zote kwako huioni tamu kwa sababu huna hamu nayo.

Mwenye kuwa na hamu na ndoa hawezi kukaa mbali na mumewe, wala kujichukulia madaraka mkononi, bali huikumbatia ndoa yake kwani hiyo ndiyo pingu ya maisha yake, kama hujawa na hamu na ndoa usiolewe. Hakuna tamu bila kuwa na hamu.


Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!