KABLA YA KUUSIKILIZA MOYO WAKO ZINGATIA HAYA

Kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.

Hayo ndiyo mapenzi jamani! lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?

Black Couple

Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.

Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.

Chunguza

Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future naye.

black-couple

Usitafute uadui

Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.

Una nafasi kwake?

Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.

black-interracial-couple

Ni rahisi kubadili uamuzi wake?

Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana future? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.


Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!