UNAUFAHAMU UMUHIMU WA KUWA NA MWENZA WA MAISHA?

Hivi umewahi kujiuliza kwanini tunakuwa na wenzi wa maisha? Kwanini mapenzi yakawepo? Kwanini wewe una mpenzi na ikitokea mkawa mmehitilafiana unakosa raha? Sina shaka kuwa katika hili, kila mmoja anaweza kuwa na fikra zake mwenyewe, lakini leo nitafafanua sababu za msingi zaidi zinazowafanya wapenzi kuwa pamoja na hatimaye kuishi katika ndoa.

Lakini kabla ya kufika mbali zaidi hebu jiulize swali moja, mapenzi humaanisha nini hasa? Kimsingi mapenzi ni hisia za watu wawili ambazo hukutana pamoja zikimaanisha upendo wa dhati. Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja wakahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo.

Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi.

Wengine hutumia nafasi hii vibaya, baadhi yao huamini kuwa ngono ndiyo mapenzi yenyewe, jambo ambalo halina ukweli. Hebu fuatilia vipengele vifuatavyo kwa makini bila shaka kuna kitu utajifunza!

KUSAIDIANA MAWAZO
Hili ni jambo la msingi zaidi katika uhusiano, mwanaume kama mwanaume, kwa uwezo wake peke yake, hata kama ana uwezo mkubwa kifedha, siyo rahisi kutimiza mipango yake ya kimaendeleo kwa uwezo wa akili yake peke yake.

Huu ni ukweli ambao wanaume wengi huukwepa kwa kuhofia kale kamsemo ka ‘tulichuma pamoja’, kimsingi unapokuwa katika muunganiko hasa kama mwenzi wako ana hekima chanya, ni wazi kuwa kutakuwa na kitu kinachoongezeka katika maisha yako. Fikra za kuwa mwanamke ni mtu wa kuzaa na kuangalia familia pekee, ni fikra za kizamani zisizo na mantiki.

VIPI KUHUSU KUKUTANA KIMWILI?
Mapenzi ni kitu kingine na ngono ni kitu kingine, ingawa baadhi ya watu hufikiria kuwa ngono ni sehemu ya uhusiano, jambo ambalo sio la kweli hata kidogo. Kimsingi ngono huja baada ya tamaa kuingia kati ya hao wawili wanaopendana!


Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!